HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 29, 2025

TASAC YASHUHUDIA UTIAJI SAINI UENDESHAJI BANDARI KAVU KWALA

 


SHIRIKAa la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) katika Udhibiti wa shughuli za Usafiri Majini leo tarehe 28 Julai, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Bandari limeshuhudia utiaji saini wa taasisi 6 juu ya taratibu za uendeshaji zitakazoratibu uhamasishaji, uhifadhi na ukabidhiwaji wa mizigo katika Bandari Kavu ya Kwala kutoka Bandari ya Dar es salaam.

Bw. Salum amesema tukio la utiaji saini linaonesha namna TASAC na taasisi hizo zinavyozingatia misingi ya Udhibiti, Uwazi na Ushirikishwaji katika maandalizi ya nyaraka za msingi.

"Tukio hili linaonesha namna mnavyozingatia misingi ya udhibiti ikiwemo uwazi na ushirikishwaji katika maandalizi ya nyaraka za msingi. Maelekezo ya kiudhibiti katika kupitia kanuni za Bandari kavu yamekuwa yakilenga kuhakikisha kuwa uanzishwaji wa Bandari Kavu unachochea ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam bila kuathiri shughuli nyingine za kiuchumi na kijamii katika jiji la Dar es Salaam". Amesema Bw. Salum.

Bw. Salum ameongeza kuwa Maelekezo hayo ya kiudhibiti ni pamoja na kuyataka maeneo ya Bandari kavu kuwa na vifaa vya kutosha kuhudumia shehena, kuwa na miundombinu ya reli inayounganishwa na maeneo ya Bandari na kuchochea uanzishwaji wa maeneo mapya ya Bandari kavu yaliyo nje ya mji katika umbali usiopungua Kilomita 30 kutoka Bandarini ili kuimarisha usalama wa Wakazi, kuondoa msongamano wa magari katika maeneo yenye shughuli nyingine za kiuchumi na kijamii katika jiji la Dar es Salaam.

Aidha, Bw. Salum amewaasa wananchi waunge mkono ili kuleta tija hasa wale ambao wanaingiza mizigo kupitia Bandari ya Dar es Salaam.

"Uhamishaji wa shehena kwenda Bandari Kavu ya Kwala una fursa ya kipekee katika kuongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam, nawaasa wananchi kuunga mkono juhudi za serikali ili kuleta tija hasa mnaoingiza mizigo kupitia Bandari ya Dar es Salaam." Amesema Bw. Salum

Taasisi zilizoshiriki katika utiaji zaini ni pamoja na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Chama cha Mawakala wa Meli Tanzania (TASAA), DP World na Tanzania East Africa Gateway Terminal Limited (TEAGL).


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad