HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, July 6, 2025

SEKTA YA USAFIRI MAJINI INATAKIWA KULINDWA NA KUDHIBITIWA -NAHODHA MANDIA

 

Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Nahodha Mussa Mandia akipata maelezo wakati  alipotembelea  Banda la TASAC  kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere 'Sabasaba' jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Nahodha Mussa Mandia akizungumza na waandishi wa Habari mara alipotembea  k Banda la TASAC  kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere 'Sabasaba' jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu 

SHIRIKA la Uwakala wa Meli (TASAC)limesema kuwa Sekta ya Usafirishaji kwa njia ya maji inachangia uchumi mkubwa hivyo inahitaji kulindwa na kudhibitiwa.

Hayo ameyasema Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Nahodha Mussa Mandia wakati alipotembelea Banda la TASAC katika Maonesho ya 49 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.

Nahodha Mandia  amesema kuwa njia ya Usafiri wa majini kinachoangaliwa ni usalama wa vyombo pamoja na mizigo inayoingia ndani pamoja na vyombo vidogo vya ndani vinavyotumia maziwa.

Amesema  kuwa katika usafiri wa bahari shehena kubwa zinazoingia ndio zinakwenda kuchochea uchumi wa nchi katika kuongeza pato la Taifa.

"Bodi tumejipanga katika kushauri katika kuona matokeo  yanaonekana katika kuendelea kulinda usalama wa vyombo vya majini pamoja na abiria katika vyombo vidogo kwenye maziwa"amesema Mandia.

Nahodha Mandia amesema Serikali ya awamu ya Sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeweza kuwekeza katika bandari mbalimbali na miradi hiyo itakuwa na matokeo mazuri katika katika kuendelea kuchochea maendelea kwa wananchi kwa uchumi wa mtu mmoja moja hadi taifa kwa ujumla.

Amesema katika Maonesho ya yanayoendelea wananchi watembelee Banda la TASAC kupata elimu kuhusu sekta ya usafiri wa majini.

Hata hivyo amesema wananchi  wanatumia vyombi vidogo katika usafiri waangalie usalama wao kwa kuwa na vifaa vya uokozi.

Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Nahodha Mussa Mandia akizungumza na waandishi wa Habari mara alipotembelea  Banda la TASAC  kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere 'Sabasaba' jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Nahodha Mussa Mandia akisaini Kitabu cha Wageni wakati  alipotembelea  Banda la TASAC  kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere 'Sabasaba' jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Nahodha Mussa Mandia akiwa katika picha za pamoja na wafanyakazi wa TASAC mara baada ya  kutembelea Banda la TASAC  kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere 'Sabasaba' jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad