Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
WATALAAM zaidi 1500 wawekimo Wanasayansi, watunga sera kutoka sehemu mbalimbali duniani wanatarajiwa kushiriki Kongamano la Kimataifa la Kilimo na Lishe linalotarajia nchini Tanzania.
Amesema katika kongamano hilo washiriki watajadili namna ya kuimarisha sekta ya kilimo na lishe duniani na kwamba limekuja wakati muafaka, kwani Serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipanga kuboresha sekta ya kilimo na kuhakikisha wananchi wanakuwa na lishe bora.
“Jambo la kushangaza ni kwamba licha ya Tanzania kuwa na mikoa inayozalisha chakula kwa wingi, bado kuna maeneo yanayokumbwa na utapiamlo au uzito kupita kiasi.”
Kwa upande wake Profesa Suneetha Kadiyala, mtaalamu wa kimataifa wa lishe kutoka LSHTM amesema kongamano hilo linatarajiwa kutoa mapendekezo ya kisera na kitaalamu yatakayosaidia mataifa wanachama kupambana na changamoto zinazoikumba sekta ya chakula na lishe, hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya tabianchi na ongezeko la idadi ya watu.
Pia amesema kongamano hilo linaunganisha nia ya kisiasa, uongozi wa kikanda na jamii ya kimataifa katika kuboresha mifumo ya chakula duniani.”Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2016, jukwaa hili limekuwa likiwakutanisha wadau mbalimbali na limechangia kwa kiasi kikubwa kusaidia watunga sera kuboresha hali ya lishe.”
Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo ulifanyika leo Juni 22,2025 jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSSAKA, MICHUZI TV)
No comments:
Post a Comment