Viongozi wa matawi ya timu ya soka ya Yanga Mkoa wa Geita wameitaka Bodi ya Ligi kujiuzulu nafasi zao kutokana na kushindwa kuendesha ligi kwa uweledi badala yake wanaendesha kwa utashi wao wenyewe bila kufuata misingi na sheria ya uendeshaji wa ligi.
Baadhi ya viongozi wa Yanga Mkoa wa Geita,Rajab Mohammed na Edmund Chrizant wamesema hayo wakati wa mkutano wa matawi ya Mkoa wa Geita iliyofanyika katika Tawi la Nyawilimilwa halmashauri ya wilaya ya Geita. Viongozi hao wa Chama wamesema hayo kutokana na mechi ya watani wa jadi Yanga na Simba inayotarajiwa kuchezwa Juni 15,2025 ikiwa ni mchezo wa 184 wa ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kuharishwa Machi 8,2025. Katika hatua nyingine wameiomba bodi ya ligi kuu kujiuzuru mara moja ili kunusuru mpira wa Tanzania huku wakiwataka Viongozi wa Yanga kutobadilisha msimamo wao.
No comments:
Post a Comment