Na Khadija Kalili, Michuzi TV
MKURUGENZI wa Rasilimali Watu na Mafunzo ya Wizara ya Afya Dkt. Saitore Laizer aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufunga mafunzo ya wahitimu kutoka Chuo Kikuu Cha MUHAS amesema amefurahishwa na tasnia hiyo kuoata mafunzo kwani katika hali ya hali ya kawaida matabibu na wataalamu wa afya hawafundishwi uongozi.
Ikumbukwe kuwa Chuo Kikuu cha Afya kilichotangulia katika sekta ya afya tunatambua mchango mkubwa wa kuzalisha watalamu wengi , MUHAS kwa wingi wake wamezalisha matabibu, famasia, wauguzi stashahada na astashahada ubingwa na bingwa bobezi, na kama taifa tumejiwekea malengo ya kupunguza kwa kiwango kikubwa cha wagonjwa wa Tanzania kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Katika uuguzi na taaluma magonjwa mengi ambayo wagonjwa wengi walikua wakienda kutibiwa nje ya nchi hivi sasa wanatibiwa nchini kutokana na Chuo kikuu cha sayansi shirikishi Muhimbili MUHAS kuzalisha wataalamu wa afya wa magonjwa hayo hivyo tumeokoa kiasi kikubwa cha fedha za kigeni.
"ikiwamo dola , unapopunguza idadi ya watanzania kwenda kutibiwa nje unapunguza matumizi ya dola, unapoongeza huduma za bingwa bobezi pia huvutia utalii wa kiafya, ndani ya Afrika Mashiki na nje ya Afrika wagonjwa wengi wanakuja kutibiwa kama MOI, KJCI tunapata wagonjwa wengi kutoka nje ya nchi hivyo tunaingiza fedha za kigeni" amesema.
Wataalamu wa nchi yetu wanatumika kwenda nje ya nchi kwenda kuwajengea uwezo madakri wa nchi za jirani, ikikwamo visiwa vya jirani wanakwenda kupeleke huduma kwa majirani sababu magonjwa hayana mipaka, tunaongeza urafiki na masuala ya kujenda diplomasia na nchi za jirani.
Magonjwa yaliyokua yanaongoza kupeleka wagonjwa nje ya nchi hasa ni moyo, mishipa ya damu, mishipa ya fahamu pamoja na ubongo yameengoza kuvutia wagonjwa kutoka nje ya nchi kuja kutibiwa hapa nchini.
Wahitimu wa mafunzo ya uongozi kutoka Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS ), wamehitimu mafunzo hayo huku wakitoa wito kwa taasisi mbalimbali kupeleka wataalamu wao ili kupata elimu hiyo.
Akizungumza kuhusu mafunzo hayo Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili MUHAS Prof. Appolinary Kamuhabwa amsema kuwa katika mafunzo hayo ya siku tatu wamefundishwa katika maeneo mbalimbali ya uongozi ambayo yatakwenda kutusaidia katika utendaji wetu wa kazi.
No comments:
Post a Comment