KWA mara nyingine tena, Meridianbet imeonesha kuwa iko pamoja na jamii – si kwa maneno tu, bali kwa vitendo. Leo hii, timu ya Meridianbet imefika katika maeneo ya Makumbusho na Mwananyamala, kwa lengo la kuwagusa wale ambao kwa namna moja au nyingine wanapitia changamoto za maisha.
Katika moyo wa upendo na mshikamano wa kijamii, Meridianbet imewafikia familia zenye uhitaji na wajane, ikiwa ni sehemu ya dhamira yao ya dhati ya kurudisha kwa jamii – utamaduni ambao kampuni hii imeendelea kuuenzi kila siku.
Kwa tabasamu na machozi ya furaha, wakazi wa maeneo hayo walipokea msaada wa vyakula na bidhaa muhimu za nyumbani ikiwemo:Mchele, Sukari, Mafuta ya kupikia, Sabuni, Unga wa sembe na ngano.
Ni msaada uliokuja kwa wakati muafaka, hasa kwa familia ambazo zimekuwa zikiendelea kupambana na hali ngumu ya kiuchumi. Kila kifurushi kilichotolewa kilikuwa ni zaidi ya msaada, kilikuwa ni ishara ya matumaini, upendo na mshikamano.
"Jamii ndiyo msingi wa kila mafanikio tunayoyapata. Leo tumefika hapa sio kwa sababu tuna mengi, bali kwa sababu tuna moyo wa kugawana na wale wanaohitaji zaidi," alisema mmoja wa wawakilishi wa Meridianbet aliyeongozana na timu katika tukio hilo.
Kwa miaka kadhaa sasa, Meridianbet imeendelea kuonesha kuwa kamari si tu burudani, bali pia ni chombo cha kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya watu. Kupitia miradi mbalimbali ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), Meridianbet imeweza kufanikisha misaada kwenye sekta za elimu, afya, michezo na sasa chakula kwa familia zenye uhitaji.
Kwa hakika, leo Makumbusho na Mwananyamala wameandika historia mpya ya upendo – historia ambayo itaendelea kuishi mioyoni mwa walioguswa.
Meridianbet – Daima na Jamii.
NB: Jisajili na Meridianbet na cheza michezo ya kasino ya mtandaoni upate ushindi kirahisi, Pia ongeza maokoto yako kwa kubashiri michezo mbalimbali yenye ODDS KUBWA. PIGA *149*10# AU tembelea tovuti yao meridianbet.co.tz
No comments:
Post a Comment