Akizungumza leo Mei 27, 2025 jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano uliowakutanisha wanachama wa Taasisi hiyo kutoka ndani na nje ya nchi, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga, amesema kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kufikia malengo ya Kitaifa ya kuwa na uchumi wa kidigitali ndani ya miaka kumi ijayo.
“Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, asilimia 33 ya Watanzania ni vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 34, ambao wengi wao wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ajira. Kupitia mkakati wa uchumi wa kidigitali uliopitishwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mwaka jana, vijana wanapaswa kuchangamkia fursa mpya za kiuchumi,” amesema Dkt. Mwasaga.
Ameongeza kuwa vituo hivyo vimekuwa msaada mkubwa katika maandalizi ya kufanikisha malengo ya Taifa na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, huku akitaja ushiriki wa wawakilishi kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Zambia na Nigeria kama mfano wa mafanikio hayo.
Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Dkt. Jabhera Matogoro, amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa vituo hivyo mwaka 2024, Wilaya ya Kondoa imeshuhudia maendeleo makubwa katika TEHAMA, ambapo shule tano zimepatiwa vifaa vya kompyuta.
“Kila shule iliyofikiwa imepata kompyuta 20 kwa ajili ya mafunzo, ingawa bado kuna changamoto ya upatikanaji wa mtandao na baadhi ya sera zinazozuia utekelezaji wa majukumu,” amesema Dkt. Matogoro.
Nao washiriki wa mkutano, Mwenyekiti wa Tarime Community Network, Bw. Gamisi Nsiko, amesema kuwa wanashirikiana na kampuni ya Vodacom katika kutoa vifaa vya TEHAMA, ambapo shule nne tayari zimenufaika.
“Shule za Sekondari zilizopokea msaada ni Mwanga Nyanyari, Serengeti na Masonge. Walimu na wanafunzi wametoa shukrani kwa msaada huo,” amebainisha Bw. Nsiko.
Naye Mwenyekiti wa Kondoa Community Network, Bi. Salama Sarungi, amesisitiza kuwa ushiriki wao katika mkutano huo ni hatua kubwa katika kufanikisha malengo yao, huku akieleza kuwa wamefanikiwa kusaidia shule za sekondari kuondokana na ufaulu wa daraja sifuri.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano uliowakutanisha wanachama wa Taasisi ya School of Community Network
kutoka ndani na nje ya nchi, leo Mei 27, 2025 Jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Dkt. Jabhera Matogoro akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano uliowakutanisha wanachama wa Taasisi ya School of Community Network
kutoka ndani na nje ya nchi, leo Mei 27, 2025 Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mwandamizi wa Programu kutoka Paradigm Initiative Bw. Ihueze Nwobilor akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano uliowakutanisha wanachama wa Taasisi ya School of Community Network kutoka ndani na nje ya nchi, leo Mei 27, 2025 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kondoa Community Network, Bi. Salama Sarung akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano uliowakutanisha wanachama wa Taasisi ya School of Community Network kutoka ndani na nje ya nchi, leo Mei 27, 2025 Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kondoa Community Network, Bi. Salama Sarung akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano uliowakutanisha wanachama wa Taasisi ya School of Community Network kutoka ndani na nje ya nchi, leo Mei 27, 2025 Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment