HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 26, 2025

AKIBA COMMERCIAL BANK YAKUTANA NA WATEJA WA MWANZA, ZAIDI YA WATEJA 250 WAHUDHURIA MKUTANO WA MAHUSIANO

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank Plc, Bw. Silvest Arumasi (katikati), akizungumza na wateja wa Benki hiyo mkoa wa Mwanza wakati wa hafla ya kukuza na kuimarisha mahusiano na wateja hao pamoja na kupokea mrejesho kwa ajili ya kufanya maboresho ya bidhaa pamoja na viwango vya huduma. wengine pichani kutoka kushoto ni Afisa Biashara Mkuu wa ACB, Bi. Wezi Mwazani pamoja na mwakilishi wa wafanya Biashara wa soko kuu la Mwanza.
Meneja wa Akiba Commercial Bank Tawi la Mwanza Bw.Emmanuel Makula akitambulisha timu yake ya ushindi ya Tawi hilo Wakati wa hafla ya kukuza na kuimarisha mahusiano na wateja wa benki hiyo mkoa wa mwanza.

Na Mwandishi Wetu
BENKI  ya Akiba imeendelea kuonyesha dhamira yake ya kuwa karibu na wateja kwa kuandaa mkutano maalum na wateja wa Mwanza uliofanyika tarehe 22 Mei 2025 katika ukumbi wa Gold Crest Hotel.

Tukio hili lilivutia zaidi ya wateja 250, ikiwa ni ishara ya hamasa kubwa na utayari wa jamii ya Kanda ya Ziwa kunufaika na huduma Benki hiyo.

Katika mkutano huo wa ana kwa ana, wateja walipata nafasi ya kuzungumza moja kwa moja na viongozi waandamizi wa benki, kutoa maoni yao kuhusu huduma, kueleza changamoto wanazokutana nazo katika shughuli za kifedha, pamoja na kujifunza kuhusu huduma na bidhaa mpya za benki.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Akiba, Bw. Silvest Arumasi, alipata nafasi ya kuzungumza na wateja na kueleza kuwa mkutano huu ni sehemu ya mikakati ya Benki katika kuimarisha mawasiliano na wateja wake. Alisema:

“Benki ya Akiba inaamini katika kusikiliza wateja wake. Lengo letu ni kuelewa vizuri zaidi mahitaji yao halisi ili tuweze kutoa huduma zinazogusa maisha yao kwa namna chanya, hasa katika mazingira yao ya kila siku.”

Bw. Arumasi aliongeza kuwa benki inaendelea kuweka mkazo katika kutoa msaada kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati kwa kuwapa jukwaa la kuzungumza moja kwa moja na wataalamu wa kifedha na kupata ushauri wa kibiashara wenye manufaa ya moja kwa moja.

Afisa Mkuu wa Biashara, Bi. Wezi Mwanzani, alieleza kuwa mwitikio mkubwa wa wateja wa Mwanza ni ushahidi wa Imani ya Wakazi wa Mwanza kwa Benki ya Akiba pamoja na uhitaji mahitaji mkubwa wa huduma za kifedha. Alisema

“Tunashukuru kwa mwitikio mzuri kutoka kwa wateja wa Mwanza. Kama benki, tutaendelea kutoa huduma bunifu na zinazolenga kumsaidia mteja katika uhalisia wa biashara zake. Mwanza ni sehemu muhimu ya mpango wetu wa kuhakikisha huduma zetu zinawafikia watu wote.”

Bi. Wezi alisisitiza kuwa dhamira ya benki ni kuijenga jamii jumuishi kifedha, kwa kuhakikisha watu wote wanapata nafasi sawa ya kutumia huduma za kifedha kama njia ya kujikwamua kiuchumi.

Mbali na majadiliano, tukio hili pia liliambatana na utoaji wa elimu ya kifedha. Wateja walielimishwa kuhusu usimamizi wa fedha binafsi na za biashara, matumizi salama ya huduma za kidijitali kama benki mtandao na miamala kwa njia ya simu, pamoja na mbinu bora za kukuza biashara kwa njia endelevu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad