Timu ya mpira wa kikapu ya wanawake, Fox Divaz kutoka Mara, imetwaa ubingwa wa Tanzania betPawa NBL, baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya BD Lioness ya Dar es Salaam.
Katika mchezo uliofanyika kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma, Fox Divaz waliibuka na ushindi wa pointi 67-54 dhidi ya BD Lioness na kutwaa ubingwa kwa mara ya kwanza.
Kwa kutwaa taji hilo, Fox Divaz walikabidhiwa kombe na zawadi ya pesa taslimu Shilingi milioni 2.8 kutoka kwa wadhamini wakuu wa mashindano hayo, betPawa.
BD Lioness, waliomaliza nafasi ya pili, walipatiwa Shilingi milioni 2.4.
Katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu, Orkeeswa walipata ushindi wa mezani kwa pointi 20-0 baada ya Viipers Queens kushindwa kufika uwanjani. Orkeeswa walizawadiwa Shilingi 700,000.Zawadi zote zilikabidhiwa na Nassoro Mungaya, Mratibu wa Masoko wa Kanda ya Afrika Mashariki wa betPawa.
Mungaya aliwapongeza wachezaji wa timu zote, maofisa, na wadau wa mpira wa kikapu kwa kujitokeza kwenye Uwanja wa Chinangali kushuhudia mechi hiyo.
Alisema betPawa inajivunia kuwa mdau wa mchezo huo na kuahidi kuendeleza juhudi za kukuza hapa nchini.
"Tumejidhatiti kukuza mchezo wa mpira wa kikapu nchini. Tumevutiwa na viwango vya wachezaji, na naipongeza timu mshindi na zingine kwa kiwango kizuri walichoonyesha katika mashindano yote huko Dodoma," alisema Mungaya.
Kwa upande wake, kocha mkuu wa Fox Divaz, Bariki Kilimba, alisema kuwa bidii na ari ya wachezaji wake ndiyo iliyowafanya kufanikisha ushindi huo.
Kilimba alieleza kuwa kila mchezo ulikuwa mgumu, lakini wachezaji wake waliweza kucheza kwa uwezo wao wa juu, jambo ambalo limewafanya wakazi wa mkoa wa Mara kujivunia.
"Wachezaji wangu wanastahili pongezi kwa ushindi huu. Walipambana sana ili kufanikisha mafanikio haya. Tumeonyesha kuwa hata vilabu vya mikoani vinaweza kuibuka na changamoto katika mchezo huu," alisema Kilimba.
"Tulicheza jumla ya mechi tisa na kushinda nane. Hili ni rekodi, na wachezaji wangu 12 pamoja na maofisa wanne walipokea Shilingi 1,260,000 kila mmoja kama Locker Room Bonus kutoka betPawa. Tumehamasika kwa zawadi hiyo," aliongeza Kilimba.
Alisema malengo yao yanayofuata ni kufuzu kwa mashindano ya Kanda ya Tano kwa mara ya pili mfululizo, kufuatia mafanikio yao ya mwaka jana.
Mratibu wa masoko wa Kanda ua Afrika Mashariki wa kampuni ya betPawa, Nassoro Mungaya akikabidhi kombe kwa washindi wa mashindano ya betPawa NBL kwa wanaume, timu ya Dar City ya mkoa wa Dar es Salaam.
Mratibu wa masoko wa Kanda ua Afrika Mashariki wa kampuni ya betPawa, Nassoro Mungaya akikabidhi kombe kwa washindi wa mashindano ya betPawa NBL kwa wanawake, timu ya Fox Divaz ya mkoa wa Mara.
Mratibu wa masoko wa Kanda ua Afrika Mashariki wa kampuni ya betPawa, Nassoro Mungaya akikabidhi mfano wa hundi kwa washindi wa mashindano ya betPawa NBL kwa wanawake, timu ya Fox Divaz ya mkoa wa Mara.
Mratibu wa masoko wa Kanda ua Afrika Mashariki wa kampuni ya betPawa, Nassoro Mungaya akikabidhi mfano wa hundi washindi wa mashindano ya betPawa NBL kwa wanaume, timu ya Dar City ya mkoa wa Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment