HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 8, 2024

WAREMBO MISS TRAVEL WORLD WATEMBELEA MIRERANI KWENYE TANZANITE

 

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Fakii Raphael Lulandala (watatu kushoto) akizungumza juu ya ziara ya warembo wa Miss Travel World 2024 walipotembelea mji mdogo wa Mirerani.

Na Mwandishi wetu, Mirerani
WANYANGE watano watakaowania umalkia wa dunia wa Miss Travel World 2024 wametembela ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, ili kujionea na kufanya utalii katika eneo hilo.

Warembo waliotembelea ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite ni Miss Travel Tanzania Agness Satura, Miss Travel Kenya Faith Amina Opurong, Miss Travel Nigeria Rosemary Johnson, Miss Travel Czech Republic Julie Hojdyszova na Miss Travel India Aarti Salunke.

Wakizungumza kuhusu ziara hiyo wanyange hao wameeleza kuwa wamefurahi kupata fursa ya kutembelea Mirerani na kuona eneo pekee duniani yanakopatikana madini ya Tanzanite.

Miss Travel Tanzania, Agness Satura amesema wamejifunza mengi ya madini hayo ya Tanzanite, kabla ya kufanyika kwa mashindano ya dunia ya Miss Travel World 2024 jijini Arusha, Agosti 9.

Mrembo huyo amesema wamefanya utalii kwenye eneo la madini ya Tanzanite ili kuweza kuyatangaza zaidi kwani kwa hapa duniani yanapatikana mji mdogo wa Mirerani pekee.

“Ni jambo zuri kutembelea eneo la Mirerani na kufanya utalii wa madini ili kujionea mahali yanakopatikana madini haya ambayo yana sifa ya kipekee,” amesema Satura.

Mnyange wa Miss Travel Kenya, Faith Amina Opurong, amesema matamanio yao yametimizwa kwa wao kufika eneo la Mirerani na kuona mahali yanapopatikana madini ya Tanzanite.

Miss Travel India Aarti Salunke, amesema ni fursa nzuri kuwa kwenye eneo linalopatikana madini ya vito ya Tanzanite ambayo ni maarufu duniani kutokana na upekee iliyonayo.

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, Fakii Raphael Lulandala amewapongeza wanyange hao kufanya utalii kwenye machimbo ya madini ya Tanzanite ili kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan.

“Kwenye filamu ya The Royal Tour Rais Samia alifika Mirerani ili kuitangaza Tanzanite kwenye utalii na pia miaka hii miwili baada ya filamu hiyo kuonekana utalii umezidi kuongezeka,” amesema.

Mkuu huyo wa wilaya amesema ziara ya warembo hao siyo kuwa ni vyema tuu kutembelea Mirerani ila ni kichocheo cha kufanya utalii eneo hilo kwani madini ya Tanzanite siyo vito vya thamani pekee ila yapo eneo la utalii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad