Nchimbi ameyasema hayo Agosti 7, 2024 alipokuwa akizungumza na maelfu ya wananchi wa Mji wa Ngara, katika Uwanja wa Posta, akiwa katika siku ya pili ya ziara yake mkoani Kagera, baada ya Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe. Ndaisaba George Ruhoro kuwasilisha kilio hicho kwenye mkutano huo.
Mapema pia kabla ya mkutano wa hadhara huo, Balozi Nchimbi alitoa maelekezo kuhusu suala hilo la upatikanaji wa vitambulisho vya NIDA, aliposimama kuwasalimia wananchi wa Kijiji cha Kumunazi alipokuwa njiani akitokea Biharamulo, kueleeka Ngara.
Akiwa ameambatana na wajumbe wa Sekretarieti ya CCM Taifa katika ziara hiyo; Ndugu Issa Haji Usi Gavu, Ndugu Amos Gabriel Makalla na Ndugu Rabia Hamid Abdallah, Balozi Nchimbi ameielekeza Wizara hiyo kuchukua hatua haraka ili changamoto hiyo imalizwe.
Amesema hata utaratibu wa kuruhusu watu kuazimana vitambulisho vya NIDA kwa shughuli mbalimbali ni jambo hatari, linaloweza kusababisha uhalifu.
"CCM itasimamia ili kuhakikisha suala hilo linafanyiwa kazi na kasi ya utoaji wa vitambulisho vya NIDA inapatikana," amesema Dk. Nchimbi.








No comments:
Post a Comment