HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 8, 2024

TIA yaandika historia Kwa kupeleka Chuo Kikuu cha Elimu ya Juu Tanga

 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Profesa William Pallangyo akizungumza na waandishi  wa Habari  kuhusiana na mikakati ya Taasisi hiyo juu ya kupeleka Chuo Kikuu cha Kwanza cha Elimu ya Juu Jijini Tanga wakati alipotembelea la Taasisi hiyo kwenye Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

TIA yaandika historia Kwa kupeleka Chuo Kikuu cha Elimu ya Juu Tanga 

Na Chalila KIbuda,Michuzi TV Dodoma 
TAASISI ya uhasibu nchini (TIA) imeandika historia kwa kuanzisha Chuo Kikuu cha Kwanza cha Elimu ya  katika Mkoa huo (Kampas)  katika Mkoa wa Tanga.

Mkoa huo ni muda mrefu ulikuwa hauna Chuo cha Elimu ya Juu licha ya kuwa na historia mzuri tangu kuanzishwa kwake.

 Akizungumza na waandishi wa habari Agost 7,2024 Jijini Dodoma kwenye maonesho ya Kimataifa ya wakulima,wavuvi na wafugaji Nanenane Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA  Profesa William Pallangyo amesema kwa mwaka huu  Taasisi hiyo imefungua Tawi na kuanza mwaka wa Masomo mwakani.

Amesema tawi ambalo wanategemea kulifungua kwamba litakua linafundisha wanafunzi kuanzia level ya cheti (basic certificate),Diploma (stashahada) pia watakuwa na shahada ya kwanza 

"Kwenye ngazi hizo tutafundisha masomo yanayohusiana na Uhasibu, Procurement and logistics, human resource management, marketing na public relations pamoja na public sector accounting, hayo ni maeneo tunayotegemea wananchi wa Tanga watafaidi kwa muda mfupi ujao",Amesema na kuongeza 

"Tumeona tutumie fursa hii pia kuwaambia wananchi wote popote walipo kwamba kuna campus mpya iliyopo Tanga na ni campus ambayo bahati nzuri pia ina hostel za wanafunzi kukaa",Amesema.

Akizungumzia kampasi ya Singida Prof.Pallangyo amesema Singida ni Mji ambao umekua na Taasisi za Elimu ya Juu lakini hauna nafasi ya kusoma shahada ya uzamili (masters) lakini  mwaka huu  wamepata bahati, serikali imeturuhusu kuanzisha shahada hiyo katika campas hiyo  ya Singida.

Amesema TIA imekua ikiona changamoto ambazo wanafunzi wanazipata hasa za kulipia ada,Taasisi kwa kuliona hilo tarehe 26 mwezi wa 10 wanategemea kuwa na  TIA MARATHON ambayo itaongozwa na Waziri wa fedha Dkt.Mwigulu Nchemba.

Amesema lengo la Marathoni hiyo ni kupata fedha ambazo zitadaidia wanafunzi.

"Kuna baadhi ya wanafunzi ambao  wamepata bahati ya kusoma sekondari lakini wanapofika vyuo vikuu wanapata changamoto za kulipa ada,  hivyo marathon yetu itakwenda kusaidia kwenye makundi makubwa mawili kundi la kwanza ni wale wanafunzi ambao hawana uwezo wa kifedha lakini kundi la pili tunawaita "young mothers" Wale wanafunzi ambao wamekuja chuoni lakini pia wana familia , wana watoto wadogo kwa hiyo ili ni kundi ambalo tumeona ni muhimu liweze kusaidiwa kuweza kusoma kwa furaha kwa maana ya kuwasaidia sehemu ya fedha ambazo watazihitaji",

Profesa Pallangyo  amesema wanatarajia mwaka huu kuwa mkutano unaoitwa Mkutano wa tatu(The third international conference on business studies) ambao utafanyika Arusha ambapo Kongamano hili tunategemea lifanyike kati ya tarehe 07 hadi tarehe 09 mwezi wa 11 hukub mgeni rasmi akitarajiwa kuwa  awe ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati  Dkt Doto Biteko.

Kwa upande wao wanafunzi ambao ni wanufaika wa chuo hiko Yusuph Mtimandole aliyebuni mfumo wa kuuza korosho(CUSHENUTZ) Mtwara na Nicolaus Mboya aliyebuni mfumo (FARM CONNECT)wamepongeza juhudi zinazofanywa na chuo hiko katika kumsaidia mwanafunzi kutimiza wajibu na kuhakikisha anakuwa fursa kwa wengine na hatimae kuendelea kuzalisha ajira nyingi kwa vijana.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad