Mwenyekiti wa Bodi ya VETA Profesa Sifuni Mchome na Wajumbe Wake wakipata maelezo Kuhusu mtambo wa kutengeneza udongo wa kuoteshea mazao ya bustani kutoka kwa Meneja Uhusiano Uhusiano wa VETA Sitta Peter wakati Bodi hiyo ilipotembelea Banda la VETA Katika Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya VETA Profesa Sifuni Mchome na Wajumbe Wake Akizungumza kuhusiana na Asali wakati Bodi hiyo ilipotembelea Banda la VETA Katika Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya VETA Profesa Sifuni Mchome na Wajumbe Wake wakipata maelezo kutoka kwa Meneja Uhusiano wa VETA Sitta Peter Kuhusiana na Asali kutoka Chuo cha VETA Dakawa wakati Bodi hiyo ilipotembelea Banda la VETA Katika Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Baadhi ya maeneo ya Banda la yakionesha Ubunifu kwa Mwenyekiti wa Bodi ya VETA na Wajumbe wakati Walipotembelea Banda hilo kwenye Maonesho ya Kilimo Kitaifa yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Yataka mashine zinazozalishwa kuongeza thamani ya kuweza kufanya biashara
Na Chalila Kibuda Michuzi TV, Dodoma
MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Profesa Sifuni Mchome amesema kuwa ubunifu na ujuzi uliopo VETA ni kuongeza dhamani ya kuweza kufanya biashara ya kuuza mashine na mitambo na bidhaa mbalimbali.
Hayo aliyasema Mwenyekiti wa Bodi Profesa Mchome wakati Bodi hiyo ilipofanya ziara kwenye Banda la VETA katika Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Amesema VETA ni Kilimo ambapo VETA inakwenda kutanzua changamoto zilizopo katika sekta ya Kilimo ,Mifugo na Uvuvi kutokana na kuwepo ubunifu wa mashine za kurahisisha sekta hizo .
Amesema VETA inaongeza kipato kutokana na ujuzi unaopatikana katika maeneo mbalimbali.
Profesa Mchome amesema VETA kupata ujuzi katika vyuo haungalii Elimu ya Juu ulionayo kwani unapata unapata ujuzi wa kufanya kufanya kazi zaidi ya moja.
Amesema Serikali imewekeza fedha nyingi kujenga vyuo ambapo vinahitaji makundi yote kupata ujuzi na Taifa kuwa na nguvu kazi yenye uzalishaji.
Amesema kuwa ujuzi wa VETA inaondoa changamoto ya ukosefu wa ajira kwa ujuzi huo kutumika kubuni na kutengeneza vitu ambavyo soko lake linakuwa la uhakika.
Profesa Mchome amesema VETA ni Mbadala wa Mambo Mbalimbali ambayo yanayoonekana changamoto kutatuliwa ikiwemo Sekta ya Kilimo baadhi ya mashine ambazo zilikuwa zikiagizwa nje ya nchi sasa zinapatikana VETA
Amesema ubunifu uliopo ni kuongeza thamani na kufanya biashara ndani na nje ya nchi kwani vitu vya VETA vinakuwa na ubora.
Aidha amesema kuwa Bodi itaendelea kushauri katika kukidhi matarajio katika sekta mbalimbali.
No comments:
Post a Comment