HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 23, 2024

CHELSEA KUZIMA NDOTO ZA ARSENAL LEO?

 


KINACHOSUBIRIWA kwa hamu kubwa usiku wa leo ni je klabu ya Chelsea itaweza kuzima ndoto za klabu ya Arsenal kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu.

Arsenal leo watakua nyumbani kumenyana na Chelsea ili kupata alama tatu muhimu ambazo zitaendelea kuwaweka kwenye mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa msimu huu, Lakini Chelsea wao watakua na nafasi ya kuweza kufanya kitu cha tofauti licha ya kutokua na fomu nzuri kwasasa.

Mchezo huu ni muhimu kwa vilabu vyote viwili kwani klabu ya Arsenal ambao ni vinara mpaka sasa wa ligi kuu ya Uingereza wao watahitaji kushinda mchezo huu kwa kiwango kikubwa ili kujiwekea mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa huo msimu huu.

Chelsea wao pia mchezo utakua muhimu sana kwao kwani wakifanikiwa kushinda mchezo huu watakua na matumaini ya kucheza michuano ya ulaya mwakani,Ambapo kama watakosa ligi ya mabingwa basi watapata Uefa Europa league au Uefa Conference League.

Suka mkeka wako kwenye michezo mikali itakayopigwa leo kwenye michuano mbalimbali barani ulaya na duniani kote. Machaguo zaidi za 1000 yapo huku lakini vile vile Turbo Cash pia ipo. Unasubiri nini sasa? Ingia meridianbet na ubashiri sasa.`

Timu hizi zinakutana ambapo Arsenal atakua na kumbukumbu ya kusimamishwa na Chelsea wakiwa na fomu nzuri kabisa na kulazimishwa sare ya mabao mawili kwa mawili, Hivo mchezo wa leo ndio utaamua ni nani mbabe wa mwenzake katika msimu huu wa 2023/2024.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad