HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 23, 2024

Profesa Malebo :Tanzania, imeendelea kuimarisha juhudi za kulinda haki za binadamu kwa raia wake

*Nchi imeruhusu uhuru wa kujieleza pamoja na
kukusanyika kwa uhuru

Mwandishi Wetu Maalum ,Marekani

Nchi ya Tanzania umetoa ujumbe wake Kwa Umoja wa Mataifa kuwa haitishi wala kukandamiza raia wake


Ujumbe huo umetolewa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO Profesa Hamis Malebo kwenye mkutano Jukwaa la kudumu la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Watu wa Asili (UNPFII) ulionza Aprili 15 na kuhitimishwa Aprili 26 unaofanyika nchini Marekani

Prof. Malebo ameueleza mkutano huo wa Umoja wa Mataifa kuwa Tanzania nchi inayofuata misingi ya sheria katika mifumo ya kiutawala.

"Inasikitikisha kwamba kongamano hilo linatumiwa vibaya kwa kupewa taarifa potofu na zisizo na ukweli kuhusu “Watu wa Asili nchini Tanzania”. amesema Prof. Malebo

Ameongeza kuwa kuwa katika Kongamano hilo alimsikiliza Mwakilishi mmoja kutoka Shirika la Watu wa Asili akiishutumu Serikali ya Tanzania kuwa inawatisha na kuwakandamiza watu wa asili”.

Profesa Malebo katika ujumbe wake alibainisha kuwa madai hayo hayana msingi na kinachofanywa ni upotoshaji kwa vitu ambavyo nchi haifanyo na haifikirii kufanya kwa wananchi wake.

Aidha Profes Malebo aliukumbusha Mkutano huo unoarekodiwa huku akiwahimiza wajumbe wa jukwaa kupitia upya rekodi za mkutano ili kujiridhisha na ukweli kuwa Serikali ya Tanzania haijatoa kauli yoyote ya vitisho wala ukandamizaji kwa raia wake.

Hata hivyo amesisitiza pia kuwa Tanzania inashiriki na kuchangia hoja mbali mbali katika mkutano huo ambapo taarifa zote zinapatikana katika jarida la Umoja wa Mataifa.

Profesa Malebo ameeleza hata katika mikutano iliyotangulia, Ujumbe wa Tanzania imekuwa ukishiriki
na kujadili hoja mbali mbali kwa uwazi kwa nia ya kujenga na kuimarisha utekelezaji wa masuala mbalimbali kwa kuzingatia haki za binadamu.

Amefafanua na kusisitiza msimamo wa muda mref wa serikali ya Tanzania na kurudia kwamba, kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Nchi yetu haina kundi maalumu la Watu wa Asili wenye haki zaidi ya wananchi wengine wala hatuna ardhi ya mababu wala ya kimila.

Prof. Malebo ameutaka mkutano huo kutambua kuwa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaongozwa kwa kufuata misingi ya utawala wa sheria na inaheshimu haki za binadamu.

Amesema Serikali haikubaliani na vitendo vya vitisho, ukandamizaji na unyanyasaji kwa raia wake, watetezi wa haki za binadamu na watendaji wengine wasio wa serikali wanaotekeleza majukumu yao kwa kufuata misingi ya utawala wa sheria.

Profesa Malebo amesema Serikali ya Tanzania inashiriki kwa lengo moja la kimataifa la utambuzi wa haki za kiraia, kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni kwa wananchi wake wote kwa kuzingatia misingi ya haki za binadamu za usawa na kutobaguliwa kwa wananchi wake na kuongeza kuwa Serikali imeweka vyombo vya utawala kwa ajili ya kukuza na kulinda haki za raia wake katika kila nyanja ya maisha. Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa uhuru wa kujieleza na hakuna vitisho wala unyanyasaji wa wananchi wanaopaza sauti zao kwa kufuata misingi ya utawala wa sheria.

Prof. Malebo amesisitiza kuwa, Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeendelea kuimarisha juhudi za kulinda haki za binadamu kwa raia wake kwa kuruhusu pamoja na mambo mengine, uhuru wa kujieleza, kukusanyika kwa uhuru na amani kwa ajili ya mikutano ya kisiasa kwa mujibu wa Katiba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad