Mkuu
wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya Tree Oceans Ltd .
Inayojishughulisha na uendeshaji wa mchezo wa kubashili wa VUNADEILE
Naseem Allan (katikati), akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi
zawadi mbalimbali kwa washindi waliojishindia kwenye mchezo wa VUNADEILE
kulia ni Mratibu kutoka BBT Vumilia Zikankura hafla yakukabidhi
zawadi hizo umefanyika jijini Dar es Salaam.Mkuu
wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya Tree Oceans Ltd .
Inayojishughulisha na uendeshaji wa mchezo wa kubashili wa VUNADEILE
Naseem Allan (kushoto), akikabidhi zawadi ya bajaji kwa mshindi wa
VUNADEILE ambapo kila wiki kunatolewa bajaji tatu wengine pichani kutoka
kulia ni Mratibu kutoka BUILDING A BETTER TOMORROW (BBT) Vumilia
Zikankura Pamoja na Meneja wa Leseni Michezo kutoka Bodi ya Michezo ya
kubahatisha nchini Lenganivo Maeti.
KAMPUNI
ya Three Oceans Ltd. Inayojishughulisha na uendeshaji wa mchezo wa
kubashili wa VUNADEILE imesema itaendelea kushirikiana na serikali
katika kuwawezesha Vijana kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na
kuwajengea uwezo wa kuweza kujiajiri.
Hayo
yamesemwa Leo Jijini Dar Salama es Salaam na Mkuu wa kitengo Cha Masoko
na Mawasiliano kutoka kwenye kampuni hiyo Naseem Allan wakati wa hafla
ya kukabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi wanaopatikana kila siku
kwenye droo ikiwemo gari mpya kabisa aina ya Toyota Ist, pikipiki, tv na
simu janja aina ya Samsung na iphone 15.
Ameeleza
kuwa katika kuendesha bahati nasibu hiyo kampuni inashirikiana na Mradi
wa kilimo ili kuhakikisha tunawawezusha vijana-BBT ni Taasisi iliyopo
chini ya wizara ya kilimo yenye lengo kuu la kutoa hamasa kwa Vijana
kujikita kwenye shughuli za kilimo biashara Ili waweze kukuza uchumi wao
binafsi na taifa kwa ujumla.
Kwa
upande wake Mratibu kutoka BBT Vumilia Zikankura amebainisha kuwa BBT
imekuwa ikiwawezesha Vijana kuingia kwenye sekta ya kilimo biashara kwa
kuwawezesha mitaji na Masoko huku akiwataka Vijana kujitokeza kwenye
program ya BBT na VUNA DEILE Ili waweze kujishindia Zawadi mbalimbali.
Tuesday, April 23, 2024

VUNADEILA KUENDELEA KUWAJENGEA UWEZO VIJANA KUJIKWAMUA KICHUMI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment