HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, April 27, 2024

BARRICK KUENDELEA KUTOA HAMASA KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KUSOMA MASOMO YA SAYANSI

 

Meneja Uhusiano wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa akikabidhi cheti na zawadi kwa mmoja wa wanafunzi wahitimu wa Shule ya Sekondari ya wasichana Kilakara aliyekuwa anafanya vizuri kitaaluma. kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Mary Lungina. Mahafali yao yamefanyika leo shuleni hapo Mkoani Morogoro.
Mgeni rasmi ambaye ni Afisa uhusiano wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa akiwa na viongozi wa shule na walimu wa shule ya sekondari ya wasichana Kilakala katika meza kuu wakati wa mahafali ya kidato cha sita shuleni hapo.


Baadhi ya wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutunikiwa vyeti.

KAMPUNI ya dhahabu ya Barrick nchini, imeeleza dhamira yake yake ya kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha elimu nchini ikiwemo kufanikisha ufaulu wa masomo ya sayansi na TEHEMA mashuleni ili taifa lisibaki nyuma katika ulimwengu wa sayansi ya teknolojia.

Hayo yamebainishwa na Meneja Mahusiano na Mawasiliano wa Barrick Tanzania, Georgia Mutagahywa katika mahafali ya wanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya wasichana ya Kilakala, iliyopo mkoani Morogoro ambapo alikuwa ni mgeni rasmi.

Alisema tayari Barrick imeanza kutoa hamasa na motisha kwa watoto wa kike wanaofanya vizuri katika masomo ya sayansi kwa kuwazawadia wanafunzi wanaofanya vizuri katika somo la hisabati na kutoa wito kwa wasichana kujiamini, kusoma kwa bidii, kuwa na nidhamu na kuondoa dhana ya kwamba masomo ya sayansi ni kwa ajili ya wavulana.

Katika jitihada za kuunga mkono jitihada za Serikali, Barrick kupitia mpango wake wa ya Kusongesha Mbele Mustakabali wa Elimu, iitwayo “Barrick-Twiga Future Forward Education Program” imetoa dola milioni 30 , (takriban shilingi bilioni 70.5 za fedha za Tanzania) kwa ajili ya upanuzi wa miundombinu ya elimu nchini Tanzania kwa ushirikiano na Serikali.

Programu ya Barick-Twiga ya Kusongesha Mbele Mustakabali wa Elimu, iitwayo “Barrick-Twiga Future Forward Education Program” inalenga kufanikisha ujenzi wa madarasa 1,090, majengo ya maliwato na vyoo 1,640 na mabweni 270 katika shule 161 nchini kote ili kusaidia kuwapatia malazi wanafunzi takribani 49,000 katika sekondari za masomo ya juu (A-level).

Kwa upande wake,Mkuu wa shule hiyo Mary Lungina,aliishukuru Serikali na wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakisaidia kuunga mkono jitihada za kuinua kiwango cha elimu nchini na alitoa rai kwa wahitimu kuongeza bidii katika kutafuta elimu zaidi ili iwasaidie katika maisha yao sambamba na kujenga Taifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad