HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 25, 2024

AIRTEL TANZANIA YANG’ARA HUDUMA BORA ZA MTANDAO-TCRA

 

AIRTEL TANZANIA imeibuka kinara wa kutoa huduma bora za mtandao kufuatia ripoti ya Takwimu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inayoishia Machi 2024 ya kila robo ya mwaka iliyochapishwa Aprili 23, 2024.

Taarifa hii ya matokeo ya kuwa kinara kwenye utoaji wa huduma za mtandao ni uthibisho wa dhamira na mikakati Madhubuti ya Airtel iliojiwekea katika kupanua huduma ili kuiweka Tanzania kwenye ulimwengu wa kidigitali. Airtel inavunja rekodi ya kuwa mtandao unaongoza kwa kuwa na simu nyingi zilizopigwa kwa robo hiyo ya mwaka kwa uwiano wa asilimia 38 (simu za Airtel kwenda Airtel) na asilimia 30 (kwa simu zilizopigwa kwenda mitandao mingine). Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya takwimu za mawasiliano zilizochapishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2023/2024.

Vilevile, ripoti hiyo inabainisha kuwa simu nyingi zaidi zilizopigwa ndani ya mtandao Airtel Kwenda Airtel zilichangia 53% ikilinganishwa na simu za nje ya mtandao 47%. Hii inadhirisha kwamba wateja wa Airtel wanaridhishwa zaidi na kupiga simu za ndani ya mtandao wa Airtel kutokana na kuwa na huduma zinazokidhi mahitaji ya wateja.

Akizungumzia matokeo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Bw. Dinesh Balsingh, alisema, “Ubunifu tulionao Airtel kwenye huduma unatufanya kuwa mtandao pendwa, gharama zetu ni nafuu na shindani, hii inawavutia wateja kuendelea kufurahia kuwa ndani ya mtao wetu. Airtel tutaendelea kutoa huduma na masuluhisho mbalimbali ili kuufanya mtandao wetu kuwa nyenzo muhimu katika kuwezesha shughuli za biashara ndani na nje ya nchi.”

Uchambuzi zaidi wa ripoti hiyo unaonyesha kuwa simu zilizopigwa na watumiaji takribani dakika 35 bilioni zilikuwa kwenye viwango bora zaidi ndani ya robo ya mwisho ya Machi 2024, ikilinganishwa na dakika 39 bilioni katika robo iliyoishia Desemba 2023. Pia imeonesha kukua kwa bilioni 4 zaidi ndani ya robo ya mwaka huo ukilinganisha na kipindi kilichopita. Kumekuwa na ongezeko la simu zinazopigwa kwa kipindi chote ndani ya mtandao.

Ripoti hiyo pia inaweka wazi uboreshaji mkubwa uliofanywa kwenye Ubora wa Huduma za mtandao wa Airtel, Airtel ikishika nafasi ya kwanza kwa asilimia 97, ikifuatiwa na Halotel kwa asilimia 94 na Tigo kwa asilimia 94.8, hivyo Airtel ikiongoza kwenye tasnia ya mawasiliano.

Bw. Dinesh alisisitiza kuwa “Airtel Tanzania tutaendelea na uboreshaji wa miundombinu ya mtandao, tutatoa huduma za kibunifu zaidi ili kukidhi mahitaji ya watanzania na wateja wetu kupitia mawasiliano. Tuna nia ya kuendelea kuiunganisha Tanzania kidigtali katika kila jambo linalohitaji huduma za mtandao.

Aidha, Airtel kwa kutajwa kuwa katika nafasi nzuri katika ripoti ya takwimu ya TCRA, Airtel inaendela kijidhihirisha kuwa lango la mawasiliano katika ukanda wa Afrika Mashariki.Pia Airtel imeweza kukamilisha mradi wa ujenzi wa Mkongo wa mawasiliano unaopita baharini wa Airtel 2Africa mwaka jana nakuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan. Airtel imejidhatiti kuendelea kutoa suluhu za mawasiliano ya simu, huduma za fedha kwa njia ya mtandao pamoja na huduma za Intaneti.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad