HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 25, 2024

Weledi wasisitizwa kwa washiriki wa Kozi Ya ICAO Ya Wakaguzi Wa Usalama Wa Usafiri Wa Anga iliyotolewa CATC

 

Washiriki Kutoka Tanzania na nchi kadhaa za Afrika waliokuwa wanahudhuria Kozi Ya ICAO Ya Wakaguzi Wa Usalama Wa Usafiri Wa Anga Inayotolewa CATC wamesisitizwa juu ya umuhimu wa kufanya kazi kwa weledi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Chuo cha CATC Godlove Longole wakati wa kufunga Kozi hiyo Machi 22,2024 jijini Dar es Salaam.

Longole ameongeza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kufanya kazi kwa maarifa, weledi na tabia njema na kusisitiza kuwa unaweza kupima maarifa na weledi wa mtu Ila ni ngumu kupima tabia njema ya mtu Ila ni muhimu kuwa nayo.

Ameongeza pia katika Usafiri wa Anga abiria wanakabidhi maisha yao kwenye taaluma ya Usafiri wa Anga kwa sababu ya weledi wao.

Jumla ya Wakaguzi 2O kutoka Tanzania na nchi nyingine za Afrika walihudhuria kozi hiyo ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO), ya wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa usafiri wa anga katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).

Kozi hiyo ya ICAO imeendeshwa na wataalam waliothibitishwa na ICAO, Bi. Millicent Henga kutoka nchini Kenya na Bi. Kagiso Mooketsi kutoka nchini Afrika Kusini .

Kozi hiyo iliyoanza Machi 18, 2024 imemalizika Machi 22,2024 na imehudhuriwa na jumla ya washiriki 20 idadi yao kwenye mabano kutoka Tanzania (11), Somalia (1), Nambia(1), Zambia(3) na Eswatini(4).

CATC moja ya vyuo vinavyotoa kozi ya Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) na ni moja ya vyuo tisa vyenye sifa hizo Afrika na 35 duniani.
Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole aliyemwakilisha Mkuu wa Chuo cha CATC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo hayo ya ICAO upande wa Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) Dar es Salaam Bw. Aristid Kanje akizungumza wakati wa kufunga kozi ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) kwa wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa usafiri wa anga inayofanyika katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC)
Mkufunzi kutoka Kenya Millicent Henga akitoa maelezo kuhusu kozi zilizofundishwa kwenye kozi maalum ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) kwa wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa usafiri wa anga inayofanyika katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).
Mkufunzi kutoka Afrika Kusini Kagiso Mooketsi akizungumza kuhusu namna chuo cha CATC kilivyoweza kusimamia kozi ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) wakati wa kozi hiyo inayofanyika katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).
Baadhi ya washiriki wa kozi ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) ya wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa usafiri wa anga wakifuatilia hotuba ya kufunga iliyokuwa inatolewa na
Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole kwa niaba ya Mkuu wa Chuo cha CATC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo hayo ya ICAO upande wa Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) Dar es Salaam Bw. Aristid Kanje.
Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole akitoa vyeti kwa washiriki wa kozi ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) ya wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa usafiri wa anga wakati wa kufungwa kwa kozi ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO)
Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole akitoa zawadi kwa Mkufunzi kutoka Afrika Kusini Kagiso Mooketsi wakati wa kufungwa kwa kozi ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO)
Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole akitoa zawadi kwa Mkufunzi kutoka Kenya Millicent Henga wakati wa kufungwa kwa kozi ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO)
Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole akiwa kwenye picha ya pamoja na wataalam waliothibitishwa na ICAO, Bi. Millicent Henga kutoka nchini Kenya na Bi. Kagiso Mooketsi kutoka nchini Afrika Kusini, wakufunzi wa CATC Dar es Salaam pamoja na washiriki wa kozi ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) ya wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa Usafiri wa Anga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad