HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 24, 2024

TCAA YATOA MKONO WA PASAKA KITUO CHA KULELEA WATOTO CHA ZILI

 

Afisa Uhusiano na Mawasiliano - TCAA Maureen Peter Swai(kushoto) akikabidhi msaada kwa Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto cha Zili House Emanuel Zadock (kulia) ikiwa ni kurudisha kwenye jamii kwakusambaza upendo na tabasamu kwa watoto yatima wa kituo hicho kilichopo eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam. Msaada uliotolewa na TCAA ni mchele, Unga, mafuta ya kula, Taulo za Kike, sabuni, ngano nk.
Afisa Uhusiano na Mawasiliano - TCAA Maureen Peter Swai akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi msaada katika kituo cha kulelea watoto cha Zili ikiwa ni kurudisha kwenye jamii kwakusambaza upendo na tabasamu kwa watoto yatima wa kituo hicho hasa kwa kipindi hiki cha Sikukuu ya Pasaka na Idd 
Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto cha Zili House Emanuel Zadock akizungumzia historia pamoja na kutoa shukrani kwa viongozi pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa kuweza kutoa msaada kwenye kituo hicho kilichopo eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam.

Dorethea ponela Daniel akitoa neno la shukrani wa viongozi pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa kuweza kuwapatia msaada kituo hicho kilichopo eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) pamoja na watoto  wakisikiliza historia ya Kituo cha kulelea watoto cha Zili House wakati wa hafla ya kutoa msaada  katika kituo hicho
 Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)  wakiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa Kituo cha Zili House pamoja na watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho mara baada ya kukabidhi msaada ikiwa ni kurudisha kwenye jamii kwakusambaza upendo na tabasamu kwa watoto yatima wa kituo katika kituo hichokilichopo eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad