HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 7, 2024

T-MARC Tanzania yafurahia ujumlishwaji wa wanawake katika nyanja mbalimbali nchini

Katika kusherehekea siku ya Wanawake Duniani, kwanza kabisa tunapongeza juhudi zinazofanywa na wanawake katika kuijenga familia, jamii, taasisi na nchi kwa ujumla wake, wakiongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dr. Samia Suluhu Hassan. Pia Tunafurahishwa sana na ujumuishwaji wa wanawake katika nyanja mbali mbali za kijamii, kisiasa na kiuchumi, ikiwemo nafasi za uongozi katika asasi, taasisi na serikali ambazo zamani zilikuwa zinashikiliwa na wanaume, hii inaonesha ni jinsi gani kama Taifa tunazingatia ujumuishwaji wa wanawake katika maendeleo. T-MARC kama taasisi ambayo imejikita katika kutoa huduma na budhaa ambazo moja kwa moja zinagusa Maisha na ustawi wa mwanamke tunatoa wito kwa wanawake wa Tanzania na duniani kote kuzidi kujiendeleza na kujiamini kuwa wanaweza kufanya chochote na kufika popote wanapotaka, na hasa wakiweka juhudi na kuzingatia kanuni za kimaendeleo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad