HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 1, 2024

DIGITAL AGENDA FOR TANZANIA INITIATIVE YATOA MAFUNZO YA UTETEZI WA HAKI ZA KIDIJITALI WA KIPEKEE NA MAKAMPUNI YA MAWASILIANO YA SIMU NCHINI



Leo, Shirika la Digital Agenda for Tanzania Initiative kwa ushirikiano na Internews na USAID, iliandaa Mkutano wa Kipekee wa Utetezi wa Haki za Kidijitali na makampuni ya mawasiliano ya simu yanayo ongoza nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na Vodacom Tanzania, Airtel Tanzania, Halotel Tanzania na TTCL Corporation.

Tukio hilo lilijadili matokeo muhimu na mapendekezo kutoka kwa Utafiti wa Uainishaji wa Haki za Kidijitali, ukilenga utawala wa kidijitali, faragha, uhuru wa kujieleza, na habari.

Akizungumza na waandishi wahabari leo Machi 01,2024 Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Digital Agenda for Tanzania Initiative Bw.Peter Mmbando amesema mkutano huo umekusudia kujenga ufahamu wa utawala wa kidijitali, faragha, uhuru wa kujieleza, na habari.

Aidha Bw.Mmbando ameeleza kuwa kupitia mkutano huo wanatarajia kuundwa kwa mfumo wa maelezo ambao utasaidia kujiondoa kwenye matangazo na kupata Suluhu pale ambapo mtandao unapokuwa dhaifu au kukwama.

Amesema faragha nyingi za wateja zimekuwa zikitumika bila idhini ya wateja au kutokuwa na sera mahususi ya kulinda data ambapo imeibua malalamiko mengi pale inapogundulika kutumika nje ya makubaliano.

"Mfumo wa utendaji wa makampuni unakusanya data nyingi sana unakuta zinatumiwa na upande wa tatu zinauzwa bila idhini ya wateja kunapokua na ulinzi wa faragha unavutia kuongezeka kwa wawekezaji wengi nchini"Bw.Mmbando amesema.

MKUTANO huo unakwenda kufanya utetezi wa kidigitali katika masuala ya faragha,uhuru wa kujieleza na kutoa taarifa kutoka kwa watoaji wa huduma hizo za mawasiliano ya simu.










No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad