Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amejumuika
na Wananchi, Viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiwemo Makamu wa Rais
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe.
Hemed Suleiman Abdulla, Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Mhe. Albert
Chalamila, Makamu Mwenyekiti CCM (Bara) Ndugu Abdulrahman Kinana, Mama
Mariam Mwinyi na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja
wa Uhuru Dar es Salaam kuaga Mwili wa Rais Mstaafu wa awamu ya pili
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi.
Shughuli
hiyo ya kuaga mwili imehudhuriwa pia na Mabalozi wanaowakisha nchi zao
Tanzania, Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Viongozi wa Dini.
Mzee
Mwinyi amefariki dunia jana tarehe: 29 Februari 2024 katika hospitali
ya Mzena, Kijitonyama, Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Friday, March 1, 2024

Home
Unlabelled
RAIS DKT. HUSSEIN MWINYI AJUMUIKA NA VIONGOZI MBALIMBALI KUAGA MWILI WA HAYATI MZEE ALI HASSAN MWINYI
RAIS DKT. HUSSEIN MWINYI AJUMUIKA NA VIONGOZI MBALIMBALI KUAGA MWILI WA HAYATI MZEE ALI HASSAN MWINYI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment