Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe, Prof. Joyce Ndalichako ameitaka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi CMA na Idara ya Kazi kutatua migogoro ya wafanyakazi kwa kuzingatia kanuni, sheria na miongozo ya serikali.
Amesema changamoto za wafanyakazi na waajiri zimekuwa zikiwasilishwa ofisini kwakwe baadala ya kufanyiwa kazi na CMA kwa kushirikiana na Idara ya Kazi ambayo ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Prof. Ndalichako amebainisha hayo leo Novemba 11, 2023 katika ukumbi wa PSSSF Mkoani Dodoma wakati wa kikao cha Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Watumishi wake na Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo.
Aidha, amezipongeza Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kufanya kazi kwa weledi, bidii na ufanisi katika kufanikisha shughuri za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baadhi ya Menejimenti ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) wakisikiliza kwa makini hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa kikao cha Waziri Mkuu na Watumishi wake na Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo leo Novemba 11, 2023 Mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment