Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akionesha ripoti ya hali ya Kilimo Afrika baada ya kuizindua katika kongamano la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF),linaloendelea kufanyika Katika Kituo Cha Mikitano cha Kimataifa cha Julius Nyerere(JICC) jijini Dar es Salaam leo Septemba 05, 2023.

Matukio mbalimbali katika kongamano la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) leo Seotemba 05, 2023.
Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
SERIKALI imeongeza bajeti ya kilimo kwa takriban asilimia 70, katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, kutoka dola milioni 120 mwaka 2021/2022 hadi dola milioni 397 mwaka 2023/24 ili kuleta chachu ya mabadiliko ya mfumo ya kilimo na chakula.
Hayo ameyasema Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango wakati akifungua kongamano la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF), Katika Kituo Cha Mikitano cha Kimataifa cha Julius Nyerere(JICC) jijini Dar es Salaam leo Septemba 05, 2023. Amesema kuwa bajeti hiyo iliyoongezeka kwa lengo la kufanya mabadiliko katika kilimo na kuwa Kilimo Biashara.
Amesema kuwa ukuaji wa sekta ndogo ya mazao kufikia mwaka 2030 iwe asilimia 10 kutoka kiwango cha sasa cha asilimia 5.4.
Mpango huo pia unalenga kuboresha huduma za ugani na kuongeza uwekezaji katika sekta ya kilimo pamoja na kuhamasisha ushiriki wa vijana katika kilimo biashara kupitia kuanzisha kilimo cha umwagiliaji wa vitalu chini ya Mpango wa Kujenga Kesho bora ambao ni Mpango wa Vijana kwa Biashara ya Kilimo (BBT-YIA).
Amesema katika mradi wa BB-YIA umefanikiwa kwa kuanzisha kituo atamizi (incubation) cha biashara kwa vijana katika chuo Cha Sokoine kiitwacho Sokoine University Graduate Entrepreneur Cooperative (SUGECO).
Pia amesema wamejenga jengo la Sekta ya Mifugo Bora Kesho (BBT-Live) kwaajili ya uzalishaji wa nyama ya ng'ombe na ufugaji wa samaki.
Dkt. Mpango amesema matokeo yameshaanza kuonekana katika Miradi hiyo licha ya kutumia teknolojia ya kidijitali kwa ajili ya kupanga, kufuatilia na kutathmini, huduma za ugani, masoko, mifumo ya malipo na huduma za usaidizi wa kibiashara.
Kongamano la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) limezinduliwa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango na linahudhuliwa na watu zaidi ya 3000 huku kukiwa na mikutano ya pembeni pamoja na maonesho ya kilimo, Ufugaji na vyakula.
No comments:
Post a Comment