Dereva wa Kampuni ya Blue Coast Vicent Kamhanda akitoa maelezo kuhusiana na mafunzo waliyopewa kutoka Chuo cha VETA Kihonda.Meneja wa Afya Usalama na Mazingira Mahala Pa Kazi wa Blue Coast Fredrick Sikayi akizungumza kuhusiana mafunzo kwa madereva wa kampuni hiyo yaliyotolewa na VETA Kihonda yaliyofanyika kampuni ya blue Coast jijini Dar es Salaam.
Mwalimu wa VETA Kihonda William Munuo akizungumza na madereva (hawapo pichani)mara baada ya kuhitimisha mafunzo katika kampuni ya Blue Coast Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi wa Magari na Mtahini wa Madereva Mkoa wa Kipolisi Temeke CPL Iman Zaidi akizungunza kuhusiana na mafunzo ya madereva wa kampuni ya Blue Coast Kigamboni jijini Dar es Salaam.
*Madereva wapongeza mafunzo kuchukua Mwalimu wa VETA Kihonda
Na Chalila Kibuda , Michuzi TV
CHUO cha VETA Kihonda Kimetoa mafunzo kwa madereva wa kampuni ya Blue Coast ya jijini Dar e Salaam ikiwa mafunzo hayo ni kujua udereva wa kujihami pamoja na kujua teknolojia ya magari.
Mafunzo hayo kwa ajili ya madereva kujihami wakiwa katika safari wakati wote pamoja na kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali.
Akizungumza mara baada ya mafunzo ya wiki mbili Mwalimu wa VETA Kihonda William Munuo amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa usalama wa barabarani pamoja na kupata elimu ya Teknolojia ya magari yanayobadilika kila wakati .
Amesema kuwa VETA Kihonda imebobea kwa udereva wa magari makubwa hivyo umekuwa ni utaratibu wa kwenda katika kampuni mbalimbali kutoa elimu ya udereva.
Munuo amesema kukiwepo kwa madereva wenye mafunzo makosa ya kibindamu yanapungua kwa asilimia kubwa ikilinganishwa na madereva wasio na mafunzo.
Aidha amesema kuwa licha ya kuwepo na mafunzo hayo amesema magari makubwa kwa teknolojia ya sasa yana umeme mwingi pamoja na upepo hivyo mafunzo kwa madereva ni muhimu.
"VETA kazi yenu ni kufikisha elimu kwa ajili ya madereva ambayo ndio kazi yetu kubwa katika kufanya madereva wasio na ajali ambapo Taifa ndio linapunguza nguvu kazi" amesema Munuo.
Mkaguzi wa magari na Mtahini wa Madereva Mkoa wa Kipolisi Temeke CPL Imani zaidi amesema kuwa katika mafunzo wamefanyisha mtihani kwa kile wanachofanya kila siku.
Amesema kuwa makosa mengi ya madereva ni makosa ya kibidamu ambapo mafunzo yanahitajika kwao.
Meneja wa Afya Usalama na Mazingira Mahala Pa Kazi wa Kampuni ya Blue Coast Fredrick Sikayi amesema kuwa mafunzo waliyopata kutoka Kihonda inaongeza tija kwenye kwenye kampuni na kuahidi kuendelea na ushirikiano wa mafunzo ya mara kwa mara.
Amesema kampuni hiyo ina magari kila aina hivyo madereva wanatakiwa kuwa na mafunzo namna ya kuyaendesha magari hayo.
Sikayi amesema kuwa dereva akiwa na mafunzo hata tatizo la gari anaweza kujieleza katika kufanya matengenezo kuliko wasio na mafunzo hawaelewi tatizo la gari lilipoanzia.
Dereva Vicent Kamhanda amesema kuwa mafunzo wanashukuru mwalimu pamoja na Menejimenti ya Blue Coast kuwapelekea mafunzo kutoka kwa mwalimu mbobevu wa magari wa VETA Kihonda.
No comments:
Post a Comment