Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kimeandaa bonanza la michezo mbalimbali kwa wafanyakazi wake ikiwa na lengo la kuimarisha afya kuwaweka wafanyakazi pamoja.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Bonanza hilo mgeni rasmi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA) Mussa Mbura amesema anawapongeza Mkurugenzi wa kiwanja, Menejimenti na wafanyakazi wote kwa kuja na wazo hili la kuandaa bonanza la michezo kwa watumishi mkiwa na lengo la kuwaunganisha watumishi, kuwajengea utamaduni wa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao na kupambana na magonjwa yasiyo ambukiza na hivyo kuchochea utimamu wa mwili na akili ili kuboresha utendaji wao. Huu ni mpango mzuri kwani michezo ni muhimu sana katika kulinda afya za watumishi wetu.
Mbura amesema kama wanavyofahamu TAA ni miongoni mwa Taasisi chini ya Wizara zinazounda timu ya Sekta ya Uchukuzi ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika mashindano mbalimbali yakiwemo SHIMIWI na Mei Mosi, hivyo kupitia program kama hizi wanaweza kujenga timu imara yenye ushindani na kuendelea kuitangaza taasisi yetu katika nyanja za kimichezo.
Amesisitiza kuwa katika mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza Serikali inahamasisha watumishi kuwa na program za michezo ili kuwawezesha kuwa na afya bora wakati wote, hivyo ufanyikaji wa bonanza hili sio tu kwa ajili ya afya za watumishi bali pia ni utekelezaji wa maelekezo ya Serikali.
“Nitoe maelekezo kwa Mkurugenzi wa Viwanja vya mikoa (DRA) kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu kusimamia program za mazoezi kwa watumishi wote hadi wa viwanja vya mikoa ili kulinda afya za watumishi wetu na kujenga timu imara zenye ushindani kimichezo. Mwakani natarajia kualikwa kwenye viwanja vya mikoa katika shughuli kama hii.” Alisema Mbura.
Pia amesema kuwa amepokea ombi la uongozi wa JNIA la kupatiwa eneo la nyuma ya jengo la VIP kwa ajili ya mazoezi, amewaomba kuwa suala amelichukua na linakwenda kufanyiwa kazi.
Naye Mkurugenzi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) Mhandisi Rehema Myeya amesema lengo la bonanza ni kuwaunganisha watumishi, kuwajengea utamaduni wa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao na kupambana na magonjwa yasiyo ambukiza na hivyo kuchochea utimamu wa mwili na akili ili kuboresha utendaji wao.
Pia amewataka watumishi wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii, nidhamu, weledi na maarifa ili kuhakikisha taasisi yetu inatekeleza vema majukumu yake iliyopewa na Serikali kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA) Mussa Mbura akikata utepe kuashria uzinduzi rasmi wa bonanza la michezo mbalimbali kwa wafanyakazi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) lililofanyika katika Viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Banana -Ukonga jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) Mhandisi Rehema Myeya.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA) Mussa Mbura akizungumza wakati wa kufungua bonanza la michezo mbalimbali kwa wafanyakazi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) lililofanyika katika Viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Banana -Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) Mhandisi Rehema Myeya akizungumza kuhusu Bonanza la watumishi wa kiwanja hicho pamoja na kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA) Mussa Mbura kwa ajili ya ufunguzi wa Bonanza hilo.
Wafanyakazi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA) Mussa Mbura alipokuwa anafungua bonanza la michezo mbalimbali kwa wafanyakazi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) lililofanyika katika Viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Banana -Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA) Mussa Mbura akipiga penati uzinduzi rasmi wa bonanza la michezo mbalimbali kwa wafanyakazi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) lililofanyika katika Viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Banana -Ukonga jijini Dar es Salaam. Aliyegolini ni Mkurugenzi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) Mhandisi Rehema Myeya
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA) Mussa Mbura pamoja na Mkurugenzi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) Mhandisi Rehema Myeya wakiongoza mazoezi kwa wafanyakazi wa kiwanja hicho cha ndege akati wa bonanza la michezo mbalimbali kwa wafanyakazi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) lililofanyika katika Viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Banana -Ukonga jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) wakifanya mazoezi wakati wa Bonanza hilo.Picha za chini ni matukio mbalimbali ya Bonanza
Bonanza likiendelea
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA) Mussa Mbura akitoa zawadi kwa washindi wa kwanza wa mpira wa miguu Kombaini wakati wa bonanza la michezo mbalimbali kwa wafanyakazi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) lililofanyika katika Viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Banana -Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA) Mussa Mbura pamoja na Mkurugenzi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) Mhandisi Rehema Myeya wakiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya mpira wa miguu Kombaini walioibuka kidedea wakati wa bonanza la michezo mbalimbali kwa wafanyakazi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) lililofanyika katika Viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Banana -Ukonga jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment