HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 30, 2023

WAKUFUNZI WA VITUO VYA KUFUNDISHIA MITIHANI YA BODI WAPIGWA MSASA

 



Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (​NBAA) imeendesha warsha kwa njia ya mtandao kwa Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia Wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi ili kuwaongezea ujuzi.

Akizungumza wakati wa kufungua warsha hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius A. Maneno amesema lengo la warsha hiyo ni kuwakumbusha majukumu yao ili kuendana na mitaala wa Bodi.

Maneno amesema mafunzo ya Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia mwaka huu yamekuja na mabadiliko ya mitaala ya masomo ya Bodi hivyo amewataka kujadili vyema ili wanapokwenda kutoa elimu wawe na uelewa mzuri.

Pia amesema lengo kubwa la NBAA ni kuona wanapandisha kiwango cha ufaulu kwa mitihani mbalimbali pamoja na kuongeza kiwango cha uelewa ili kipindi wanapomaliza mitihani yao waweze kuwa wabobezi kwenye masuala ya Uhasibu na Ukaguzi.

Amewaasa Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia masomo ya Bodi kuendesha masomo kwa njia ya mtandao ili kuweza kupunguza gharama za uendeshaji, kuwafikia wanafunzi wengi na kuendana na teknolojia.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA CPA Pius Maneno (katikati, waliokaa) akiwa pamoja na baadhi ya wakufunzi na maofisa wa NBAA wakati wa kufunga warsha ya wanafunzi na wakufunzi wa mitihani ya NBAA iliyofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 29 na 30 Agosti 2023. Kushoto ni Meneja wa Idara ya Elimu na Mafunzo NBAA, Peter Lyimo na kulia ni Mtaalamu wa Sarafu Mtandao, CPA Sandra Chogo
Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka akiwakaribisha Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia Wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi ambao walikuwa wakifuatilia Warsha hiyo kwa njia ya mtandao.
Mkufunzi CPA Ansbert Kishamba akitoa mafunzo kuhusu mbinu nzuri za kufundishia na namna ya kuweza kupitia maudhui ya mitaala hasa kwenye B5 na C1 wakati wa warsha ya Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia Wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi
CPA Douglas Munah akitolea ufafanuzi vipengele muhimu vya kitaalamu vinavyotakiwa kupewa mwanafunzi anayetegemea kufanya mitihani ya Bodi wakati wa warsha ya Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia Wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi.
Mkufunzi CPA Rashid Mganwa akitoa maelezo kuhusu mabadiliko ya masomo ya B2,B3, B4, C3 na C4 kwa Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia Wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi waliokuwa wanafuatilia warsha kwa njia ya mtandao.
Mtaalamu wa Sarafu Mtandao, CPA Sandra Chogo akitoa elimu kuhusu Sarafu Mtandao kwa Wakufunzi wa Vituo vya kufundishia Wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi waliokua wanafuatilia warsha kwa njia ya mtandao.
Afisa Idara ya Elimu na Mafunzo (NBAA), Salimu Kasumari akitolea ufafanuzi baadhi ya maswali yaliyokuwa yanaulizwa na Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia Wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi.
Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, CPA Dkt. Emmanuel Christopher akitoa elimu kuhusu njia bora ya kusimamia vituo vya vya kufundishia kwa Wakufunzi wa Vituo waliokuwa wanafuatilia kwa njia ya mtandao.
Mkufunzi kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Indiael Kaaya akitoa maelezo kuhusu namna ya kuwatengenezea mazingira mazuri ya kufaulu Wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi ili kuweza kuongeza ufanisi kwenye taaluma ya Uhasibu.
Meneja wa Idara ya Elimu na Mafunzo NBAA, Peter Lyimo (kulia) akitoa mrejesho kuhusu maboresho ya mtaala mpya wa masomo ya mitihani ya Bodi kwa Wakufunzi wa Vituo vya kufundishia waliokuwa wanafuatilia warsha kwa njia ya mtandao. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius A. Maneno.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius A. Maneno akizungumza wakati wa kufunga warsha ya Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia Wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad