Mkurugenzi wa Tiba Asili kutoka Wizara ya Afya, Profesa Pascal Rugajo Akizungumza leo Agosti 30, 2023 wakati wa kufungua kongamano la pili la kisayansi na Maonesho ya dawa za tiba asili. Kongamano hilo limefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
HOSPITALI saba kuanza kutoa dawa za tiba za asili kwa wagonjwa wenye matati mbalimbali ya afya, mgonjwa atachagua dawa za kutumia kutokana na tatizo alilo nalo.
Hospitali hizo zitakazotoa dawa za tiba asili ni kulingana na kanda ni hospitali ya rufaa ya jijini Dar es Salaam ya Temeke, Morogoro, Dodoma General, Mwanza Sekou Toure, Arusha Mount Meru, Tanga Bombo na Mbeya
Akizungumza leo Agosti 30, 2023 Mkurugenzi wa Tiba Asili kutoka Wizara ya Afya, Profesa Pascal Rugajo wakati wa kufungua kongamano la pili la kisayansi na Maonesho ya dawa za tiba asili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa Hospitali hizo zimechaguliwa kwa kufuata kanda pia wamesha toa mafunzo kwa watoa huduma watatu kwa kila hospitali.
"Dawa zaidi ya 19 zinaenda kutumika kutibu, Mgonjwa atafika kwa daktaria taonwa kwa njia ya kisasa mwisho ataambiwa kunadawa za tiba asili na zawa za kizungu Mgonjwa atachagua." Amesema Prof. Rugajo.
Amesema kuwa wameshaanza kutoa tiba kwa kutumia dawa za asili na mpaka sasa hakuna madhara yaliyojitoleza lakini wanaendelea kufanya utafiti ili kuhakikisha watanzania wanatumia tiba asili ambazo ni salama na zimethibitishwa zikiwa na mchango mkubwa katika kuendeleza tiba asili hapa nchini.
Ametaja magonjwa yanayoweza kupatiwa dawa za tiba asili katika hospitali hizo kuwa ni pamoja na vidonda vya tumboni, pumu, ngozi, upumuaji, magonjwa ya njia ya mkojo, magonjwa ya tumbo, kuungua moto na hata maumivu wakati wa hedhi.
Kwa Upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Profesa Said Aboud amesema taasisi yake inaendelea kukamilisha utafiti wa dawa ya asili ya kushughulikia tatizo la tezi dume kwa wanaume.
Amesema serikali inaendelea kufanya uwekezaji mkubwa wa afya, chini ya wizara ya afya na inapongeza jitihada zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kuendelea kuboresha sekta hiyo.
Amesema kupitia kongamano hilo, wadau wa tiba asili, wakiwemo washiriki zaidi ya 200 watakuwa na maazimio ya namna ya kuboresha eneo la tiba asili, kutoa elimu lakini pia kuongeza utafiti ili kuhakikisha watanzania wanatumia dawa salama na zilizothibitishwa.
Amesema wataendelea kuhakikisha kuwa tiba asili zinaendelezwa na tayari wapo madaktari, wauguzi pamoja na wafamasia ambao wamepatiwa mafunzo kuhusiana na huduma hizo shirikishi.
Kuhusu dawa za asili kuwa na madhara amesema, hakuna dawa isiyokuwa na madhara hata zile zisizokuwa za asili nazo zina madhara, kubwa ni mgonjwa kufuata masharti kutoka kwa wahusika.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Tiba asilia Wizara ya Afya Dkt. Vumilia Liggie amesema, dawa za asilia katika Hospitali za umma zitaendelea kuongezeka kulingana na tafiti zinazofanyika
“Kwenye hizi hospitali ukimaliza mchakato wote wa kuonana na daktari, ukifika kwenye hatua za dawa, mgonjwa ana uamuzi wa kuchagua dawa aitakayo,” amesema Dkt. Liggie na kuongeza kuwa zipo nchi za nje kama China na India ambao wanaelndelea kutumia dawa hizo.
Kongamano hilo la pili la dawa asilia limewakutanisha wataalamu mbalimbali wakiwemo watunga sera, watumiaji wa dawa, watengenezaji, wanasayansi watafiti na Wanazuoni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Profesa Said Aboud Akizungumza leo Agosti 30, 2023 wakati wa kufungua kongamano la pili la kisayansi na Maonesho ya dawa za tiba asili. Kongamano hilo limefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa dawa za tiba asili na dawa asili wakiwa katika kongamano la pili la kisayansi na Maonesho ya dawa za tiba asili. Kongamano hilo limefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Profesa Said Aboud Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 30, 2023 wakati wa kufunguzi kongamano la pili la kisayansi na Maonesho ya dawa za tiba asili. Kongamano hilo limefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment