HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 30, 2023

Vijana 763 Wahitimu Awamu ya Kwanza ya Mafunzo ya programu ya BBT

 JUMLA ya Vijana 763 wahitimu wa awamu ya kwanza ya mafunzo ya programu ya Jenga Kesho iliyo Bora (Build a Better Tomorrow - BBT), wametembelea eneo la mashamba ya pamoja ‘block farm’ lililopo Mlazo, Ndogowe ambapo watapatiwa na Serikali mashamba na maeneo ya makazi.


Eneo hilo ambalo lipo kwenye hatua ya maandalizi ni moja ya maeneo ambayo Wahitimu hao watakabidhiwa ardhi na hati kila mmoja kwa muda wa miaka 66.

Mratibu wa programu ya BBT, Bi. Vumilia Zikankuba amebainisha kuwa katika eneo hilo la Ndogowe zimepatikana hekari takribani 11,453 ambazo hazijawai kutumika katika shughul za kilimo.

Aidha, Mhe. Haruni Lucas Diwani wa Kata ya Mhambako, Mlazo ameipongeza Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mradi huo wa BBT na ameahidi kutoa ushirikiano unaotakiwa.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad