Manispaa
ya Tabora imeanza rasmi leo Agosti 28,2023 kutumia mfumo wa E-MIKUTANO
katika vikao vyake ili kuwapa fursa wajumbe wa vikao hivyo kushiriki
kikamilifu hata kama wapo nje na Manispaa.
Katika kikao cha
Morning Session cha leo, wajumbe kadhaa waliweza kushiriki kwa mfumo wa
mawasiliano ya njia ya video ( Vedeo Conferencing) akiwamo Ndugu Pius
Haule (Mkaguzi wa Ndani), Ndugu Robert Matungwa ( Mwanasheria ), Ndugu
Nelson Mwankina( Mchumi), Injinia Asteria Shija ( Mhandisi wa Manispaa)
pamoja na Ndugu Syliverster Mhumpa ambae ni Afisa Ugavi wa Manispaa.
Malengo
mahsusi ya mfumo wa E-MIKUTANO ni kuwezesha watumishi na Viongozi wa
Serikali kuhudhuria vikao vya msingi na vya kisheria bila kuwa na
kizuizi cha umbali walipo.
Hivyo Manispaa ya Tabora kuanza
kutumia mfumo huu katika vikao vyake kwanza ni kuleta tija kwenye vikao
husika kwani wajumbe watatoa mawazo, ushauri na maoni yao badala ya
wawakilishi wao ambao wangehudhuri vikao hivyo na ukizingatia
wawakilishi siku zote hawana maamuzi na hata ushauri wao huwa haupewi
uzito sana ukilinganisha na wajumbe husika.
Sambamba na mfumo
huu, vilevile Manispaa ya Tabora imeshaachana na matumizi ya Kablasha
kwenye vikao vyake, hii ikiwa inachagizwa na matumizi ya Vishikwambi
pamoja na Mfumo wa TEHAMA wa uendeshaji wa vikao vya Serikali (E-BOARD).
Hivyo Manispaa ya Tabora imeweza kununua Vishikwambi kwa idadi ya Wakuu wa Sehemu, Vitengo pamoja na Waheshimiwa Madiwani.
Kwa
ujumla wake sasa, ukiunganisha uwepo wa Vishikwambi ambavyo ni vya
kisasa kabisa, uwepo wa mfumo wa E-BOARD unaowesha upatikanaji wa
taarifa na nyaraka muhimu mtandaoni , pamoja na mfumo wa E-MIKUTANO
ambao unawesha mtumishi ama kiongozi kuhudhuria kikao kwa mawasiliano ya
njia ya video, basi vyote hivi vinaifanya Manispaa ya Tabora kutokuwa
mstari wa nyuma katika matumizi ya teknolojia ya mtandao.
Matumizi
haya ya Teknolojia ya Mtandao kwaujumla wake yanaongeza tija sana
katika utekelezaji wa dira ya Halmashauri pamoja na maelekezo mahsusi
ya Serikali kwani Mtumishi ama kiongozi anafanya kazi zake na kuhudhuria
vikao muhimu vya maamuzi akiwa popote pale.
Monday, August 28, 2023
Home
HABARI
MANISPAA YA TABORA YAANZA RASMI KUTUMIA MFUMO WA E-MIKUTANO KUWEZESHA WAJUMBE WALIOKO MBALI KUSHIRIKI
MANISPAA YA TABORA YAANZA RASMI KUTUMIA MFUMO WA E-MIKUTANO KUWEZESHA WAJUMBE WALIOKO MBALI KUSHIRIKI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment