Na Mwandishi Wetu, Tabora
MKURUGENZI
wa Manispaa ya Tabora Elias Mahwago Kayandabila amechaguliwa kuwa
Katibu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Mkoa wa Tabora.
Amechaguliwa
katika nafasi ya Katibu wa Jumuiya hiyo kwenye kikao cha ALAT Mkoa wa
Tabora kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua.
Aidha
wajumbe wa kikao hicho kwa pamoja kabla ya kikao walitembelea miradi
mitatu ya maendeleo inayotekelezwa wilayani humo na kuridhishwa na hatua
za utekelezaji.
Miradi iliyotembelewa ni ujenzi wa shule mpya
ya Mkoa (Tabora Girls Grand School wenye thamani ya Sh.bilioni 3),
ujenzi wa zahanati kwa ufadhili wa TFS na ujenzi wa maduka stendi kuu ya
Kaliua.
Pamoja na mambo mengine kikao hicho kimemshukuru Rais
Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha kwa ajili ya shule ya wasichana
mkoani Tabora.
Monday, August 28, 2023
MKURUGENZI MANISPAA TABORA ELIAS KAYANDABILA ACHAGULIWA KATIBU WA ALAT MKOA WA TABORA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment