HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 12, 2023

Tume za Kurekebisha Sheria Tanzania na Zanzibar zimesaini mkataba wa ushirikiano

Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, Jaji mstaafu, January Msoffe ( wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha Sheria Zanzibar, Khadija Shamte Mzee (wa pili kulia), wakisaini mkataba wa ushirikiano baina Tume ya Tanzania bara na Zanzibar. KusoroHafL hiyo imefanyika leo Julai 12, 2023 jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya kurekebisha sheria bara, Griffin Mwakapaje n kushoto ni Katibu Mtendaji wa Tume ya kurekebisha sheria Zanzibar Musa Kombo 

Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, Jaji mstaafu, January Msoffe akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ushirikiano kati ya Tume ya kurekebisha Sheria Zanzibar na Tume ya kurekebisha sheria Bara.
Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, Jaji mstaafu, January Msoffe ( wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha Sheria Zanzibar, Khadija Shamte Mzee (wa pili kulia), wakionesha mkataba wa ushirikiano baina Tume ya Tanzania bara na Zanzibar. KusoroHafL hiyo imefanyika leo Julai 12, 2023 jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya kurekebisha sheria bara, Griffin Mwakapaje n kushoto ni Katibu Mtendaji wa Tume ya kurekebisha sheria Zanzibar Musa Kombo.
Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha Sheria Zanzibar, Khadija Shamte Mzee akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ushirikiano baina ya Tanzania bara na Zanzibar. HafL hiyo imefanyika leo Julai 12, 2023 jijini Dar es Salaam.

TUME za Kurekebisha Sheria Tanzania na Zanzibar zimesaini mkataba wa maeneo ya kushirikiana utakaowawezesha kushughulikia changamoto za kisheria zinazojitokeza katika nyanja mbali mbali kama vile uchumi, Ulinzi, haki za binadamu na mazingira

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini ushirikiano huo leo Julai 12,203 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, Jaji mstaafu, January Msoffe amesema kuwa ushirikiano huo pia utawezesha kushughulikia masuala muhimu ya kisheria ambayo yanahitaji juhudi za pamoja.

"Ushirikiano huu ni hatua madhubuti ya kuimarisha mifumo ya sheria na kuboresha maisha ya watanzania kwa kuimarisha ubora wa upatikanaji na ufikiwaji wa sheria hizo" amesema Msoffe

Aidha Jaji Msoffe amesema kupitia ushirikiano wao wataweka mazingira wezeshi kwa ukuaji wa uchumi, uwekezaji na umoja na mshikamano ndani ya kijamii hivyo, wanaamini mfumo thabiti wa kisasa wa kisheria ndio msingi wa jamii yenye haki na ustawi.

Alisema kuwa ushirikiano kati ya tume hizo unathibitisha kuimarisha mfumo wa kisheria unaozingatia utawala bora na utawala wa sheria kwa maendeleo ya jamii.

"Ushirikiano huu utakuwa jukwaa muhimu la kubadilishana ujuzi, utaalamu na mbinu bora katika nyanja ya mageuzi ya sheria katika nchi, tutatumia nguvu zetu ili kuimarisha utafiti wa kisheria, mapitio na tathmini ya sheria zilizopo na kubainisha maeneo mbalimbali yenye changamoto na kujitahidi kuondoa upungufu au mapengo yanayoweza kuwepo kati ya mifumo ya sheria. "Amesema Jaji Msoffe.

Naye, Khadija Shamte Mzee, Mwenyekiti wa tume hiyo amsema kuwa bado umuhimu wa tume hizo haujaonekana katika jamii hivyo wanapaswa kubadilisha mtazamo.

Mzee amesema mpaka sasa wao kama Tume wanaonekana mzigo katika utekelezaji wa majukumu yao hivyo kwa kushirikiana watahakikisha wanafanya mabadiliko na kupunguza gharama ili kutimiza matakwa ya serikali.

Ameongeza kuwa ni wakati wa kuongeza kasi ya utendaji kazi wao wa kufanya mapitio ya sheria, kubadilisha na kutafiti zitumike kwenye jamii na serikali ione huduma zao.

Akielezea mkataba huo, Katibu Mtendaji wa tume Zanzibar, Mussa Kombo Bakari amesema mkataba huo una maeneo 10 ambayo ni kuimarisha ushirikiano baina ya tume hizo.

Pia kubadilishana taarifa ikiwemo ripoti za utafiti na nyaraka, kufanya tafiti za pamoja, kubadilishana utaalamu na uzoefu baina ya pande zote.

"Mkataba huu utaongeza utaalamu katika uandishi wa sheria na miswada. Itaundwa timu ya kuratibu na kutekeleza hati hii na kushauri, kuhakikisha usiri na mawasiliano," alisema Bakari.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad