HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 12, 2023

DKT. TAX APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO ZA BALOZI MTEULE WA PAKISTAN NCHINI

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amepokea nakala za hati za utambulisho za Balozi Mteule wa Pakistan hapa nchini, Mhe. Siraj Ahmad Khan katika hafla fupi iliyofanyika leo tarehe 12 Julai 2023 katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.


Katika mazungumzo yao, Mhe. Dkt. Tax amemkaribisha nchini Mhe. Khan na kumuahidi ushirikiano kutoka kwake binafsi, Wizara na Serikali kwa ujumla wakati wote atakaokuwa nchini akiiwakilisha nchi yake.

Aidha, amesema kuwa, ushirikiano kati ya Pakistan na Tanzania ni mzuri na utaendelea kuimarika kupitia Balozi Khan kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake.

Naye Mhe. Khan ameeleza furaha yake kuwa Tanzania na kwamba yupo tayari kutekeleza majukumu yake ya uwakilishi kwa kushirikiana na Wizara na Serikali kwa ujumla kwa maslahi mapana ya nchi hizi mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Pakistan nchini Mhe. Siraj Ahmad Khan. Hafla ya makabidhiano imefanyikatarehe 12 Julai 2023 katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Mhe. Dkt. Tax akimsikiliza Mhe. Khan wakati wa mazungumzo yao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad