HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 12, 2023

KAMPUNI YA DPO PAY YAPATA LESENI TANZANIA KUTOA HUDUMA ZA MALIPO

 

  Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV


KAMPUNI DPO Pay inayoongoza kwa huduma za malipo ya kidijitali imetambuliwa na kupewa kibali na Benki Kuu ya Tanzania (BoT )kutoa huduma za malipo nchini.

Kwa mujibu wa DPO Pay yenye makao makuu yake nchini Kenya, ni kwamba itaendeleza shughuli zake nchini baada ya kuwa imetambuliwa kwa mujibu wa sheria na kupata leseni.

Akizungumza leo jijini Da es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa DPO Pay, Bi Janeth Upendo Kwilasa amesema wanafurahi kupokea leseni hiyo kutoka Benki Kuu ya Tanzania ( BoT).

Amesema kwa kuzingatia dhamira yao thabiti ya kuongeza wigo wa utoaji huduma zao katika nchi za Afrika Mashariki, kibali hicho ni sehemu ya kuonesha nia yao na uthabiti wao wa kufuata taratibu zote za kisheria na kiutaratibu katika kuendesha shughuli zao nchini Tanzania.

Akieleza zaidi amesema DPO Pay ambayo sasa ipo chini ya shirika la Network International, shirika ambalo ni mwezeshaji mkuu wa biashara za kidigitali katika eneo la Afrika Mashariki na Kati iko tayari kutoa huduma zake nchini Tanzania.

Janeth amebainisha utayari wa DPO Pay katika kuchagiza na kuwezesha ujumuishaji kifedha kwa makundi mbalimbali na ustawi wa biashara kidigitali.

Amesema mifumo ya DPO ni thabiti na inawahakikishia watumiaji wake kama wafanyabiashara kufanya miamala kwa urahisi, ufanisi, uhakika na haraka zaidi huku ikihawakikishia watumiaji wake ulinzi wa taarifa zao.

“DPO Pay ina mifumo thabiti inayohakikisha ulinzi wa taarifa za mtumiaji na ubora wa huduma. Kwa kutumia DPO Pay Mobile inayopatikana (istore/playstore), wateja wetu wanauhakika wakupata huduma mbalimbal katika ubora na upekee,” amesisitiza Janeth.

Aidha amesema DPO Pay tayari inafanya kazi Zanzibar na kutumiwa na wafanyabiashara wa hoteli, usafiri na watu binafsi kuupokea na kufanya malipo kupitia DPO Pay.Huduma za DPO Pay zinatoa fursa kubwa kwa wafanyabiashara, na watu binafsi kuendesha malipo kidigitali ndani na nje ya nchi.

"Kwa sasa DPO Pay inaendesha shughuli zake katika nchi 20 barani Afrika. Pia kupitia DPO Pay, mteja anaweza kufanya malipo kupitia kadi ya benki, simu, kuhamisha fedha.",ameeeleza Janeth.

Mkurugenzi Mtendaji wa DPO Pay, Bi Janeth Upendo Kwilasa akifafanua jambo wakati akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) leo Julai 12,2023 jijini Dar es salaam kuhusu kupewa kibali (Leseni) na Benki Kuu ya Tanzania (BoT ) chakutoa huduma za malipo nchini


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad