HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 22, 2023

SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU NYERERE YAWAFUNDA VIONGOZI 71 WANAWAKE NCHINI 'SIWOLEMA'


Balozi wa Afrika kusini nchini Noluthande Mayende Malepe akiwasilisha mada kwenye mafunzo ya Viongozi  Wanawake. 

Mwakilishi mkazi wa UNDP nchini Tanzania Christine Musisi akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo Viongozi Wanawake nchini katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere.

Na Khadija Kalili Michuzi Tv
SHULE ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani imetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Viongozi Wanawake 71 wa nafasi za juu SIWOLEMA za Uongozi kutoka Tasisi za Umma, sekta binafsi na Taasisi zisizo za kiserikali nchini ili waweze kujiamini katika nafasi mbalimbali za Uongozi walizopewa.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo ya siku tano ya kuwajengea uwezo Viongozi hao Wanawake nchini katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere huku washiriki wake wametoka CRDB, NMB, NSSF, TTCL, PSSF, Mkombozi Bank, USAF, TAMESA.

Mkuu wa Shule hiyo Prof. Marceline Chijoliga amesema kuwa mafunzo hayo yamewakutanisha na kuwajengea uwezo viongozi wanawake wa ambao wanauzoefu wa uongozi siyo chini ya miaka mitano yamefanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini ambapo pia wamefundishwa mbinu bora za Uongozi wa Utawala Bora katika Taasisi wanazoongoza.

Amesema kuwa mafunzo hayo kwa Viongozi wanawake Mameneja yamefanyika Julai 17 hadi 22 , 2023 ikiwa ni muendelezo wa mafunzo mbalimbali yanayotolewa na Shule ya Uongozi kwa kushirikiana na taasisi za Umma, sekta binafsi, taasisi zisizo za kiserikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Amesema kuwa changamoto kubwa inayowakabili Vuongozi Wanawake wengi ni kutojiamini katika nafasi zao za Uongozi walizoaminiwa Serikalini na kwenye Taasisi mbalimbali za umma na binafsi ambao hudiriiki hata kukubali kuwapisha wanaume madarakani.

"Wanawake wengi ni wasomi wazuri na wanauwezo wa kufanya kazi nzuri katika nafasi walizoaminiwa lakini kwa kutojiamini kuongoza hukubali waongozwe na wanaume"

"Wapo Wanawake wanaambiwa tunakupa nafasi hii wanaogopa kuchukua ile nafasi ukimuuliza sababu anasema mimi siwezi, unamuuliza mbona umesoma sawa kushika nafasi hiyo hakubali"

"Sisi wanawake ni waajabu sana tunaweza kupata hizo nafasi lakini tukawa tayari kufanya kazi kwa kusaidia kiongozi mwanaume ambaye mnalingana kiwango cha elimu.

Amesema kuwa kuna baadhi ya Wanawake hata kujiendeleza kielimu hawataki kwa kigezo cha majukumu ya familia hivyo hata Kuna baadhi ya vyeo hawezi kufikia hivyo mafunzo haya wanewajengea uwezo viongozi hao Wanawake kwamba nini wafanye kwenye majukumu yao ya familia na majukumu ya kazini.

Prof. Chijoliga amesema kuwa mafunzo haya yamelenga kuwasaidia nini wafanye katika uongozi maana tunaaamini mwanamke kiongozi akiendelezwa atasaidia familia yake kwa kuwa kiongozi bora zaidi bali na anakuwa kiongozi bora katika mazingira yake ya kazi"

Ameyataja masomo waliyofundishwa kuwa ni pamoja na uzalendo ambao huwapa kujitambua kuwa wao ni waafrika hivyo tunawajibu wa kuhakikisha Afrika inabadilika, utawala bora kwani wanawake tunaaminika ni waaminifu hivyo tunaendelea kupanda mbegu ya uaminifu kwa wanawake wengi zaidi.

"Ikiwa ni pamoja na kuendesha miradi ya maendeleo, kujiamini, kushirikiana na wenzao kazini ikiwa ni pamoja na kufanya majadiliano ya wanawake kwa

Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini Tanzania, Christine Musisi, akifunga mafunzo hayo ya uongozi kwa viongozi wanawake amesema Shirika la Umoja wa Mataifa la Programu ya Maendeleo Tanzania UNDP linapongeza juhudi kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya sita chini ya Uongozi imara wa Rais wa kwanza mwanamke Mama Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa Uongozi wa wanawake na ushiriki wao katika ngazi za maamuzi katika ngazi zote za maamuzi serikalini.

"Tunatambua ongezeko la idadi ya viongozi wanawake bungeni, taasisi za umma na katika ngazi mbali mbali za utawala serikalini"

"Tunapongeza wanawake majasiri ambao wame onyesha umahiri mkubwa na ujasiri katika kufanya maamuzi yanayo husu Taifa, familia na jamii inayo-wazunguka pamoja na changamoto nyingi za kijinsia, kifamilia, kiuchimi na kihisia zinazo-wazunguka tofauti na wanaume"

"Hakika mwanamke akiwa katika kiti cha maamuzi basi ni rahisi kuundwa sera, mikakati na mipango inayo-wanu-faisha wanawake wengi zaidi na mwanamke akifanikiwa kiafya, kielimu na kiuchumi basi jamii na Taifa kwa ujumla litakuwa limefanikiwa"

Amesema UNDP Tanzania itaendelea kushirikiana na taasisi za serikali zinazotoa mafunzo ya Uongozi kwa wanawake kama Mwalimu J.K Nyerere Leadership School, Uongozi Institute pamoja na taasisi zisizo za kiserikali kama vile Tanzania Gender Network Program na sekta binafsi ili kuchangia ongezeko la idadi ya wanawake wenye uwezo na ujasiri wa kuongonza na kushawishi mabadiliko chanya ya kiuchumi, kisera na kijamii hapa nchini.

Balozi wa Africa kusini nchini Noluthande Mayende Malepe amesema kupinga ubaguzi wa rangi na mapambano ya kupata uhuru ilikuwa ni kipaumbele katika nchi yao lakini anafurahishwa na hatua kubwa ya Tanzania kutoa nafasi ya juu kabisa kwa mwanamke kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Baadhi  ya washiriki wa mafunzo ya Uongozi kwa Viongozi Wanawake nchini kutoka Taasisi mbalimbali nchini SIWOLEMA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad