HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 22, 2023

CHUO KIKUU MZUMBE; UDAHILI WA WANAFUNZI BADO UNAENDELEA

 

Baadhi ya wanafunzi wakipata huduma katika banda la Chuo Kikuu Mzumbe katika maonesho ya Vyuo Vikuu yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Wiliam Mwegoha akipokea cheti cha Kushiriki Maonesho ya 18 ya Vyuo Vikuu leo Julai 22, 2023 yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Nchini wakati wa kufunga maonesho hayo yaliyokuwa yakifanyika katika Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam 

CHUO Kikuu Mzumbe kimesema zoezi la udahili bado linaendelea kwa  upande wa programu za degree ya kwanza hadi pale dirisha la kwanza la usajili la Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), litakapofungwa rasmi Agosti 4, 2023.

Ameyasema hayo Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Wiliam Mwegoha leo Julai 22, 2023 alipotembelea Banda la Chuo Kikuu Mzumbe wakati wa kufunga maonesho ya 18 ya Vyuo Vikuu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) katika Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam. Amesema pia Kwa upande Programu za Astashahada na Stachahada na Cheti amesema kuwa udahili unaendelea na programu za umahiri na Uzamivu unaendelea na udahili mpaka Oktoba Mwaka huu.

"Niwaombe wanafunzi baada ya tarehe hiyo dirisha litafungwa na baadae tutafanya machakato wa kwenda kuchagua wale ambao watakuwa wamepita kwenye dirisha la kwanza, kwahiyo kabla ya dirisha halijafungwa kwa wale ambao bado hawajatembelea Wavuti au Tovuti ya Chuo Kikuu Mzumbe na kwa wale ambao watafanya udahili wafanye kwa kupitia portal ya Chuo hicho.

Akizungumzia kuhusiana na waliokosa fursa ya kutembelea katika banda la Mzumbe amesema kuwa udahili utaendelea mpaka Agosti 4, 2023.

Pia ameomba Wanafunzi wanaotaka kujiunga na Chuo Kikuu Mzumbe kuwa huru kupiga simu ili muweze kusaidiwa pale inapotokea changamoto yeyote.

Pia amesema kuwa programu zinazotolewa na chuo Kikuu Mzumbe zinamanufaa makubwa kwa hiyo wazazi na wanafunzi wasisiste kutembelea website (tovuti ) ya Chuo Kikuu Mzumbe ili waweze kujiunga na chuo hicho.

Akizungumzia programu ambazo ni maarufu amesema programu za degree ya kwanza au ya awali ya shule ya sheria na umaarufu wake umekuwepo kutokana na kufundisha kwa vitendo ndio maana wanafunzi wanaipenda.

"Vijana wanapoenda shule ya sheria yaani 'Law School' wanafanya vizuri kutokana na programu hiyo kuwa ya miaka mitatu na mwaka wa mwisho wanafundisha kwa vitendo zaidi.

Programu nyingine ni ile ya Utawala na menejiment hii ni mhimu na nguzo kwani wanawajengea uwezo viongozi na kwa wale ambao hawatakuwa viongozi inakuwa rahisi kupata ajira, wanachukuliwa sana kwenda kujitolea kwenye taasisi mbalimbali kupitia huko wanapata ajira." Amesema Prof. Mwegoha.

Eneo jingine ambalo chuo Kikuu Mzumbe ni Mahiri ni programu za biashara amesema kuwa wanafundisha wahasibu, wataalamu wa Fedha pia wanafundisha watu wa manunuzi.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Chupo Kikuu Mzumbe wakitoa huduma kwa wanafunzi waliotembelea banda lao.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad