HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 13, 2023

SERIKALI YATOA MILIONI 560 KUJENGA SEKONDARI MPYA MBINGA

 

Na Albano Midelo,Mbinga

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan Imetoa zaidi ya shilingi milioni 560 kupitia program ya Uboreshaji Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kujenga sekondari mpya wilayani Mbinga.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Amina Seif amesema sekondari hiyo mpya inajengwa katika Kata ya Matarawe ambapo ujenzi wake utahusisha vyumba vinne vya madarasa,ofisi moja ya walimu,jengo la utawala,maabara tatu, maktaba, chumba cha TEHAMA,vyoo,kichomeaa
taka na tanki la maji.

Hata hivyo Seif amebainisha kuwa Halmashauri hiyo hivi karibuni imepokea jumla Shilingi Milioni 655,552,827.00 kati ya fedha hizo shilingi 560,552,827 ni kwa ajili ya ujenzi wa sekondari mpya ya kata ya Matarawe na shilingi milioni 95 ni kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu ya
familia mbili katika sekondari ya Lusonga.

“Kwa niaba ya wananchi wa Mbinga,namshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutuletea fedha za kuboresha miundombinu ya elimu katika Halmashauri yetu hali ambayo itasaidia kuboresha elimu ya awali,msingi na sekondari’’,alisema.

Ameahidi kusimamia matumizi ya fedha hizo na kuhakikisha mradi wa ujenzi wa miundombinu hiyo ya elimu unakamilika kabla ya Oktoba 30,2023.

Serikali kupitia program ya SEQUIP katika wilaya Mbinga imetoa zaidi ya shilingi bilioni 1.8 kujenga shule mpya za sekondari katika kata za Lusonga,Amanimakoro na MataraweMradi wa ujenzi wa sekondari mpya ya Kata ya Lusonga katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga ambapo seriikali kupitia program ya SEQUIP imetoa zaidi ya shilingi milioni 560 kutekeleza sekondari hiyo ambayo imeanza kuchukua wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka huu.
Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbinga Mji Amina Seif akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani  ikwemo serikiali kutoa fedha za kujenga sekondari mpya kupitia prorgam ya SEQUIP,,kushoto aliyekaa ni Mwenye kiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mheshimiwa Kelvin Mapunda.
Baadhi ya wanafunzi wa sekondari ya Kata ya Lusonga mjini Mbinga wakiwa wameanza masomo yao mapema mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad