HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 13, 2023

WAZIRI UMMY MWALIMUA ALIA NA MADAKTARI WANAOTOA TAARIFA ZA FARAGHA ZA WAGONJWA

 


Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amemuelekeza Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu kushughulikia maadili ya kitabibu kwa madaktari wanaokiuka taratibu za kitabibu na kutoa taarifa za faragha za wagonjwa hadharani.

Waziri Ummy ametoa maelekezo hayo kufuatia taarifa iliyotolewa na Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sokoine Lindi, Dkt. Baraka Steven kuzungumzia faragha ya mgonjwa kinyume na maadili ya kitabibu ambayo inaelekeza taarifa za mgonjwa ni siri.

Kufuatia taarifa iliyotolewa na mtandao wa EATV, wadau mbalimbali waliibuka na kujadili iwapo ni sahihi kwa daktari kuzungumza na vyombo vya habari kuelezea faragha za mgonjwa bila ridhaa yake.

“Faragha ya mgonjwa ni moja kati ya sheria kuu chache za taaluma ya afya, hapa tuna taarifa zote za mgonjwa kuanzia jina, umri, jinsi yake, makazi na ugonjwa wake, tumeweka taarifa zake za siri kuwa taairfa ya habari” alihoji Bwana Sales Nicco.

“Upo sawa, hii ni kinyume na ethics za kitabibu. Namuelekeza Mganga Mkuu wa Serikali kulifuatilia na kunipatia Taarifa” amesema Waziri Ummy Mwalimu akimjibu Bwana Nicco.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad