HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 18, 2023

MAMA MZAZI WA MBUNGE WA MORO MJINI ABOOD AFARIKI DUNIA, AZIKWA MAKABURI YA KISUTU JIJINI DAR

 

 MKUU wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima ameongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Mama mzazi wa Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdul Azizi Abood aliyezikwa Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.


Akizungumza kwa niaba ya wakazi wa Mkoa wa Morogoro Mkuu wa Mkoa Adam Malima amesema msiba huo umebebwa na watu wa Morogoro kwa uzito mkubwa kutokana na mbunge huyo kubeba majumkumu mengi ya wakazi wa Morogoro wanapopatwa na matatizo kama hayo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mikumi mkoani Morogoro Denis Londo alisema wao kama wabunge wameuzunishwa na kusikitishwa na msiba huo wa mama wa mwezao na wao kama wabunge wapo pamoja katika kipindi hiki kigumu.

Baadhi ya wabunge waliokuwepo kwenye mazishi ya Mama wa Mbunge Abood ni pamoja na Mbunge Gairo Ahmed Shabiby.

Akizungumza baada ya mazishi mbunge wa Morogoro mjini Abdul Azizi Abood amewashukuru wabunge ndugu, jamaa na marafiki wa familia kwa kuwa pamoja naye katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na Mama yake mzazi. "Tumempumzisha Mama katika makaburi ya Kisutu."

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad