HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 20, 2023

TOASTMASTERS INTERNATIONAL WAKUBALIANA KUSHIRIKISHA WADAU ZAIDI WA MAENDELEO KUBORESHA SEKTA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI

 
Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

WADAU mbalimbali kutoka sekta binafsi pamoja na serikalini wameshiriki kwenye kikao cha mazungumzo yaliyoandaliwa na Shirika la ToastMasters International ambacho kimeanza leo Mei 19,2023 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Mei 19,2023 jijini Dar es Salaam baada ya kufunguliwa kwa kikao hicho cha siku ya kwanza cha ToastMasters ambao kwa mara ya kwanza unafanyika Afrika Mashariki na hasa Tanzania, Kiongozi wa ToastMasters Kanda ya Mashariki Emilia Siwingwa amesema wameanza vikao vya mkutano mkuu wa mwaka na utaendelea kwa siku mbili.

“Katika kikao chetu cha kwanza ambacho tumeshirikisha wadau kutoka sekta binafsi pamoja na serikali sambamba na wanachama wetu wa Afrika Mashariki, mengi tumezungumza kwa lengo la kuhakikisha tuaendelea kuboresha sekta ya biashara na uwekezaji.

“Tumezungumza na kujadiliana kwa kina na miongoni mwa mambo ambayo tumeyaangali ni je tunafanya maendeleoe endelevu? Je kwenye uwekezaji tuko wapi lakini pia tukiangalia na upande wa biashara.Katika maeneo yote lazima unamuangalia mwanadamu, je anauwezo gani, ana ujuzi gani wa kuweza kuhakikisha maendeleo yanatekelezwa.”

Akifafanua zaidi amesema yeye ni Wakili wa kujitegemea lakini alichobaini huwezi kuendelea bila kuwa na uwezo wa kujielezea , kuwasiliana na watu ili ukisema wanakuelewa na wewe ukisikia kitu unakielewa , hivyo kwenye mazungumzi ya leo wamejadili kwa kina mambo hayo.

Pamoja na mambo mengine, amesema wametoka na mikakati mipya ambapo wamekubaliana kwamba iko haya ya kuendelea kuzungumza na kushirikisha Serikali katika masuala yanayowezesha kuimarisha sekta ya biashara na uwekezaji sambamba na kusaidia jamii kuwa na maendeleo.

“Tumekubaliana haya mazungumzo lazima yaendelee kwani yanagusa maslahi ya wanadamu,kwa hiyo tumekubaliana tuendelee kuzungumza , tuilete Serikali karibu ili tuweze kufikia mikakati itakayoweza kusaidia wananchi.

“Katika ya sekta ya biashara , katika sekta ya uwekezaji, huwezi kupata mafanikio , huwezi kuboresha sekta ya biashara bila kuna na watu ambao wanapata uelewa zaidi , kwa hiyo leo tulikuwa na watalaamu mbalimbali ambao wametusaidia kutungea uelewa zaidi na hivyo tulivyokuja ni tofauti na tulivyoondoka.”

Kuhusu wanachama wa ToastMasters nchini Tanzania amesema idadi yao sio kubwa ukilinganisha na nchi kama Kenya lakini wamebaini huenda hakujakuwa na hamasa kubwa zaidi lakini kupitia kikao cha leo kuna idadi kubwa ya watu wameomba kujiunga, hivyo matarajio yao wataendelea kuongezeka siku hadi siku.
Rais wa Shirika lisilo la kiserikali TOASTMASTERS INTERNATIONAL Matt Kinsey akifafanua zaidi kwa namna gani mkutano huo wa kwanza wa mwaka wa shirika hilo ambao kwa mara ya kwanza unafanyika Afrika Mashariki na hasa Tanzania, umekuwa wa muhimu katika kuwashirikisha wadau wa Maendeleo kuboresha sekta ya biashara na uwekezaji katika nyanja mbalimbali ambako shirika hilo limekuwa likihudumu
KIONGOZI wa Shirika lisilo la kiserikali Kanda ya Afrika Mashariki TOASTMASTERS INTERNATIONAL, Emilia Siwingwa akizungumza na Wageni waalikwa mbalimbali walioshiriki mkutano wa kwanza wa mwaka shirika hilo ambao kwa mara ya kwanza unafanyika Afrika Mashariki na hasa Tanzania,ambapo amesema wameanza vikao vya mkutano mkuu wa mwaka na utaendelea kwa siku mbili jijini Dar es Salaam.

Mijadala mbalimbali kutoka kwa Wadau wa maendeleo ya biashara na uwekezaji ilitolewa katika mkutano huo

Baadhi ya wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ndani ya mkutano huo muhimu kwa shirika hilo la TOASTMASTERS INTERNATIONAL
Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad