HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 18, 2023

.RAIS SAMIA AZINDUA RASMI MRADI WA MINARA YA KURUSHA MATANGAZO YA TELEVISHENI (DTT) AZAM MEDIA

 NA EMMANUEL MBATILO MICHUZI TV

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amezindua Mradi wa Minara ya Kurusha Matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni ya Azam Media Limited ambao umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 50 za Kitanzania ambao utahakikisha kuwa na uhakika wa matangazo ya Televisheni nchini.

Akizungumza katika  hafla hiyo ambayo imefanyika leo Mei 18,2023 katika Viwanja vya Azam  Media Hub Jijini Dar es Salaam,Rais Samia amesema minara hiyo  ambayo imezinduliwa itaifanya nchi kuwa ya kwanza katika teknolojia ya 5G ambayo itatupatia huduma kiganjani bila kuwa na line ya simu ambayo ni mageuzi makubwa nani jambo la kujivunia kama Taifa.
 
"Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu namna ya sekta ya habari ianvyokwenda hapa nchini, nimefarijika kuona hi sasa kumekuwa na mwelekeo mzuri baada ya utekelezaji wa maagizo ambayo nilimpa Waziri na tumi yake wakati namwapisha, uhusiano baina ya vyombo vya Serikali na vyombo binafsi lakini na Wizara umeimarika sana". Amesema 

Aidha amesema Serikali imejipanga kuja na Satellite ambayo itaweza kusaidia wananchi kupata mawasiliano na habari kwa haraka katika ikiwemo kutambua utekelezaji unaofanywa na Serikali na mengine yanayoendelea nchini na ulimwenguni kote. 

"Wote tunakumbuka kuwa nchi yetu iliachana na mfumo wa analojia katika matangazo ya Televisheni na kutumia teknolojia ya digitali tangu Juni 17, 2015, hatua hii ilikuwa ni utekelezaji wa makubaliano ya kimataifa kutokana na faida nyingi kama vile ubora wa picha na sauti matumizi bora ya masafa ya utangazaji, na nishati ya umeme, uwezekano wa kutoa huduma za ziada kama internet na matumizi ya runinga za mkononi na kwenye magari, Tanzania ilifanikisha mpango huu ndani ya muda uliopangwa".Amesema Rais Samia.

Amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kuhakikisha uendelevu wa sekta ya habari kwa upande wa teknolojia ya utangazaji " na nimejulishwa  kuwa mwaka 2021, Wizara ya Habari ilifanya mapitio ya mfumo wa leseni na udhibiti wa sekta ndogo ya utangazaji ili kuwezesha mazingira ya utendaji kazi katika sekta hiyo".

Pamoja na  hayo Rais Samia amesema vyombo vya habari vipo huru kusema na kuandika wanayoyataka, muhimu kufuata mila na desturi zetu nchini, hilo ni muhimu sana, mila na desturi zetu nchini ni kuheshimiana, vyombo viheshimu na vyenyewe viheshimiwe.
 
"Uhuru maana yake ni kujiendesha wewe mwenyewe na kujiweza na kujitegemea, ndipo utakapokuwa huru, lakini kama unataka kuwa huru kusema, kesho unarudi Serikalini tubebe tusaidie, ili tuweze kusema, hapana uhuru hapo, sasa kama vyombo vya habari vinataka kuwa huru, viweze kujiendesha vyenyewe kama inavyojiendesha Azam". Ameeleza.

Sanjari na  hayo ameipongeza timu ya Yanga kwa kuweza kuingia fainali kwenye michuanoya Kimataifa hivyo amewasihi watanzania kuendelea kuiunga mkono timu hiyo ili iweze kupata nguvu na kuweza kufanikiwa kushinda finali.

"Sasa niseme yafuatayo, nilianza na mechi hizi na Milioni 5 kwa kila goli la ushindi, waliposogea nikasema sasa milioni 10 kwa kila goli la ushindi, tunapokwenda kwenye fainali ni milioni 20 timu ikitoka na ushindi, milioni 20 hii haitakwenda kufungwa mbili kafungwa moja, hapana, yawe magoli yote yameipa timu hii ushindi, kila goli milioni 20". 

Vilevile amesema  Serikali itatoa ndege, kuwapeleka katika mchezo wa fainali na ndege hiyo itabeba wachezaji pamoja na mashabiki, "na naomba sana wale viongozi wa TFF na mchezo huu, kuwapa moyo kama Serikali tunavyofanya".

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye amesema Mradi huo utasaidia kuongeza wigo wa wananchi kufikiwa na matangazo ya televisheni na hivyo kuongeza kuwawezesha kupata taarifa muhimu kuhusiana na masuala mbalimbali yanayoendelea hapa nchini ikiwepo utekelezaji wa sera, program na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali.

Amesema Sekta ya Habari hapa nchini ni kati ya sekta ambazo zinakua kwa kasi hasa baada ya hatua kadhaa ulizoagiza zichukuliwe ulipoingia madarakani miaka miwili iliyopita, hatua hizo zimeifanya sekta ya Habari nchini itulie na hivyo kuongeza mchango wa sekta katika kuimarisha nchi yetu.

"Tunatarajia zoezi la mapitio ya sera hii litafanyika kwa haraka ili sekta hii ya utangazaji iendelee kukua kwa kuzingatia misingi ya sera, tupo katika hatua za mwisho za mapitio na tutafuata mchakato wa kuirekebisha sera hii". Amesema Waziri Nape.

Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Bw. Tido Mhando amesema Mradi huo wa DTT umesheheni miujiza ya kuweza kufanikisha utangazaji na maendeleo ya baadae ya matangazo ya 5G ambapo channel za Televisheni zitaweza kuonekana moja kwa moja kwenye simu yako ya mkonini bila kupitia kwenye App kama ilivyo hivi sasa.

"Uwekezaji mkubwa sana wa Azam Media wa zaidi ya shilingi Bilioni 225.6 kwa kipindi cha miaka 10 kwenye ligi kuu ya Tanzania ni kiasi kikubwa tu lakini si kiasi ambacho tunaweza kusema kimeweza kuonesha mafanikio makubwa katika nchi hii, uwekezaji huu hivi sasa umeanza kuzaa matunda, leo hii watanzania wapenda maendeleo na furaha ya kitaifa wamejaa tabasamu na bashasha kufurahia ushindi wa jana wa Klabu ya Yanga kufanikisha kwa mara ya kwanza kwa soka la Tanzania kuingia fainali ya michezo ya CAF". Amesema Bw.Mhando

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kufungua Mradi wa Minara ya Kurusha Matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni ya Azam Media Limited leo Mei 18,2023 katika Viwanja vya Azam Media Hub Jijini Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Minara ya Kurusha Matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni ya Azam Media Limited leo Mei 18,2023 katika Viwanja vya Azam Media Hub Jijini Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya kifaa maalum cha kuangalia matangazo ya Azam TV akiwa kwenye gari lake akiwa mahali popote kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Limited Bw. Abubakar Bakhresa katika uzinduzi wa Mradi wa Minara ya Kurusha Matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni ya Azam Media Limited leo Mei 18,2023 katika Viwanja vya Azam Media Hub Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na mtoto Georgina Magesa mwenye ndoto za kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyekutana nae leo katika uzinduzi wa Mradi wa Minara ya Kurusha Matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni ya Azam Media Limited leo Mei 18,2023 katika Viwanja vya Azam Media Hub Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akimruhusu mtoto Georgina Magesa kuketi kwenye kiti chake, mtoto mwenye ndoto za kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,aliyekutana nae leo katika uzinduzi wa Mradi wa Minara ya Kurusha Matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni ya Azam Media Limited leo Mei 18,2023 katika Viwanja vya Azam Media Hub Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mstaafu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Kate Kamba katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Minara ya Kurusha Matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni ya Azam Media Limited leo Mei 18,2023 katika Viwanja vya Azam Media Hub Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Minara ya Kurusha Matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni ya Azam Media Limited leo Mei 18,2023 katika Viwanja vya Azam Media Hub Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua studio za Azam Media Limited katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Minara ya Kurusha Matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni ya Azam Media Limited leo Mei 18,2023 katika Viwanja vya Azam Media Hub Jijini Dar es Salaam.

( PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)


 
 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad