HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 22, 2023

NBAA YATOA MAFUNZO SHULE YA SEKONDARI YA TURIANI

 


Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka akitoa elimu pamoja na kuwahamasisha wanafunzi kujiunga na masomo ya Uhasibu watakapomaliza masomo ya Sekondari katika Shule ya Sekondari ya Turiani iliyopo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Afisa Masoko na Mawasiliano wa NBAA, Magreth Kageya akitoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Turiani iliyopo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Turiani wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) waliofika kutoa elimu pamoja na kutoa msaada wa vitabu vya masomo ya Biashara na hisabati.
Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka akimkabidhi Mkuu wa Shule Msaidizi Hamidu S. Sudi kwa niaba ya Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Turiani vitabu vya masomo ya Biashara pamoja na hisabati vipatavyo 300 ikiwa ni kurudisha kwa jamii kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa NBAA. Wa kwanza kulia ni Mwalimu Isdola Sawele na wa kwanza kushoto ni Afisa Masoko na Mawasiliano wa NBAA, Magreth Kageya.
Afisa Masoko na Mawasiliano wa NBAA, Magreth Kageya (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Shule Msaidizi Hamidu S. Sudi kwa niaba ya Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Turiani vitabu vya masomo ya Biashara pamoja na hisabati vipatavyo 300 ikiwa ni kurudisha kwa jamii kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa NBAA. Wa kwanza kulia ni Mwalimu Isdola Sawele.
Baadhi ya wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wakiwa kwenye picha ya pamoja na  baadhi ya Walimu wa Masomo ya Biashara pamoja na wanafunzi wanaosoma masomo ya biashara mara baada ya kutoa msaada wa vitabu 300 pamoja na kutoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo na jinsi ya kufanya mitihani ya Bodi.
Baadhi ya vitabu vya masomo ya Biashara na Hisabati vilivyotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika shule ya Sekondari ya Turiani jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad