HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 22, 2023

MAHAFALI YA 12 YA KIDATO CHA SITA SHULE YA ST. JOSEPH CATHEDRAL DAR YAFANA, WAZIRI DKT. GWAJIMA ATOA NENO

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima akitoa vyeti kwa wahitimu wa kidato cha sita wa shule ya St. Joseph ya jijini Dar es Salaam mwshoni mwa wiki.


 WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amesema serikali imekuwa ikifanya kampeni mbalimbali ili kuunganisha makundi mbalimbali kwenye jamii ili kupunguza matukio ya ukatili na mmomonyoko wa maadili nchini.


Ameyasema hayo wakati wa mahafali ya 12 ya Kidato cha Sita ya chule ya St. Joseph Cathedral iliyopo jijini Dar es Salaam Mei 21,2023. Amesema kuwa watanzania wanaitikia kufanya kampeni hizo hadi mtu mmoja mmoja anasimama anafunga mtaa wake.

"Msione kujenga majengo haya ndio mmemaliza kazi, msione kununua magari haya ndio mmemaliza kazi, msidhani kutokukaa na watoto na kudhani kwenda kukaa meza ndefu ndio mmemaliza kazi.... Chunga sana Mtoto wako maana shetani anaajenda nae." Amesema Dkt. Gwajima

Pia amewaasa wahitimu hao kulindaa sana mioyo yao na wakeshe wakiomba na kulinda watoto kuliko vyote walivyonavyo.

Dkt. Gwajima amewaasa kuzingatia maelekezo ya walimu, wazazi na walezi katika maisha ya kila siku, lakini amesisitiza maelekezo mema ndio wazingatie zaidi kwa sababu kuna baadhi ya wazazi wanachangamoto ya malezi, makuzi na maadili hawa ni wale pengine hawakulelewa na wamepata neema ya kuzaa sasa watakuja kuleaje huyu mwingine.

"Hali hii tumwombe Mungu sana atufunulie ufunuo wa wakati wa sasa ili kila anae leta mtoto duniani awe ameandaliwa kifikra katika suala la Malezi na makuzi." Amesema Dkt. Gwajima

Amesema kuwa wanaoenda vyuo vikuu nako shetani ameshapaharibu ndio maana Serikali imeweka madawati ya kijinsia, Madawati ya ulinzi wa watoto kwa sababu takwimu zinasema kama hukukatiliwa shuleni basi huko wanakoenda.

Pia amewaasa wawe wa kidijitali kimioyo na ishikamane na Mungu maana huo ndio ulinzi pekee.

Mkuu wa Shule ya St. Joseph Cathedral, iliyopo jijini Dar es Salaam Sister Theodora Faustine amesema wahitimu 230 wamemaliza masomo yao huku akiiomba Serikali na wadau wengine kutazama upya na kunusuru malezi ya watoto wa kiume leo kwani hali si shwari na limeshakuwa tatizo kubwa katika jamii.

"Hali ya mmomonyoko wa maadili isipotazamwa kwa haraka ni hasa italeta hasala kwa taifa." Amesema

Kwa upande wa Mzazi, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mureba, Oska Kikoyo amewaasa wanafunzi wa Shule hiyo kufuata mafundisho wanayoelekezwa shuleni hapo na waende kuyatumia vyema nyumbani na vyuoni.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima akitoa vyeti kwa wahitimu wa kidato cha sita wa shule ya St. Joseph ya jijini Dar es Salaam mwshoni mwa wiki.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza wakati wa mahafali ya 12 ya shule ya St. Joseph ambapo wahitimu 230 walitunukiwa vyeti vyao kwa mwaka 2023.


Matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 12 ya shule ya St. Joseph Cathedral ya jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima akitoa zawadi ya fedha kwa mwalimu wa ngoma katika shule ya st. Joseph Cathedral.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad