HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 17, 2023

DART kujenga Chuo cha Mafunzo ya Udereva wa BRT

 

Mkurugenzi Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala na Kaimu Mtendaji Mkuu wa DART. Eliphas Mollel akizungumza kuhusiana na ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Udereva wa Mabasi yaendayo haraka (BRT) wakati wa semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari , jijini Dodoma

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV Dodoma
WAKALA wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) umesema kutokana na ukubwa na umuhimu wa Mradi wa DART, unatarajia kuanzisha Chuo cha Madereva wa Mabasi yaendayo haraka (BRT) nchini.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa DART, Dkt. Eliphas Mollel wakati wa mafunzo ya Mradi wa DART kwa Waandishi wa Habari yanayofanyika Dodoma kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu mradi huo ili wakaweze kuhuhabarisha vyema umma wa Tanzania.

Dkt Mollel amesema pamoja na mambo mengine chuo hicho kitafundisha madereva wa mabasi yanayohudumu katika mradi huo kwani mradi utarajiwa kuwa na madereva 6000 ambao ni muhimu kuandaliwa mahususi kwaajili ya BRT.

“Pindi Mradi wa DART utakapokamalika na kuanza kutoa huduma katika awamu zote sita, unatarajia kutoa ajira kwa madereva takribani 6000. Idadi hii ni kubwa hivyo ni muhimu kuandaliwa kwa kupatiwa mafunzo ya kuhudumu katika BRT”, alisema Dkt. Mollel.

Aidha Dkt. Mollel amesema tayari Wakala wa DART umeshafanya maombi ya eneo kutakakojengwa chuo hicho ambacho kitakuwa Manispaa ya Kigamboni na maendeleo yake yanakwenda vizuri.

Dkt. Mollel amesema Mradi wa DART umekuwa ukipokea wageni mbalimbali kutoka nchi za Afrika ambao wanakuja kujifunza kuhusu uendeshaji wa mabasi yaendayo haraka kwa matarajio ya kwenda kuanzisha katika nchi zao na madereva watakuja kusoma kwani Chuo hicho kitakuwa cha kwanza Afrika.

Amesema uwepo wa chuo hicho mbali na kuhudumia madereva wa Mradi wa DART, pia utasaidia nchi nyingine kuleta watu watu wao kuja kujifunza mambo ya BRT na hivyo kuingizia mapato nchi pamoja wakala huo.

Dk.Mollel amesema sifa za kusoma ni zilezile za nchi hivyo mafunzo hayo ni kwa ajili ya mabasi yaendayo haraka ambayo yataongeza ujuzi wa namna ya uendeshaji wa abiria kwa viwango vinavyohitajika katika mradi huo.

Amesema kuwa hiyo ni fursa kwa Watanzania wote na ni wakati sasa kwa madereva wanawake kujiandaa kuendesha mabasi yaendayo haraka kwani idadi ya madereva wanawake katika mradi ni ndogo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad