Tamasha la Raha za Pwani kufanika Machi 11, 2023 Zanzibar - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 4, 2023

Tamasha la Raha za Pwani kufanika Machi 11, 2023 Zanzibar


TAASISI ya Doris Mollel inayoshughulika na masuala ya kusaidia watoto njiti, Kwa kushirikiana na Mwanamitindo wa siku nyingi wa hapa nchini, Khadija Mwanamboka wameandaa Tamasha Kubwa la Burudani lililopewa jina la " Raha Za Pwani 2023" ambalo linatarajia kufanyika Machi 11, 2023 huko visiwani Zanzibar likiwa na lengo la kupata fedha za kusaidia vifaa tiba kwa ajili ya kusaidia watoto Njiti, visiwani humo.

Tamasha hilo, litawakutanisha wanamuziki wakongwe wa muziki wa taarab wakiongozwa na Malkia Khadija Kopa, Sabaha Salum Muchacho, Leyla Rashid na Mc Du, Ambao watapanda Jukwaani siku hiyo kukonga nyoyo za wapenzi wa taarab asilia na fedha zitakazopatikana kutokana na viingilio, zitapelekwa kwenye vifaa tiba kwa ajili ya watoto njiti Zanzibar.

Tamasha hilo linakwenda sambamba kabisa na maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Dunia ambayo huadhimishwa kila ifikapo Machi 8, ya kila mwaka Duniani kote.

Mgeni rasmi katika tamasha hilo, anatarajiwa kuwa ni Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad