HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 2, 2023

MBUNGE WA NGO's AOMBA WANAWAKE KUPEWA ELIMU JUU YA MATUMIZI SAHIHI YA TEKNOLOJIA

Mbunge wa Viti Maalumu anayewakilisha Asasi za Kiraia(NGO's) Neema Lugangira, na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi wakiwa katika Picha ya pamoja na wanavyuo mbalimbali Machi Mosi jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Viti Maalumu anayewakilisha Asasi za Kiraia(NGO's) Neema Lugangira, na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi wakiwa katika Picha ya pamoja.

Na Avila Kakingo, Michuzi TV
WANAWAKE ili waweze kujikomboa kwenye suala la teknolojia lazima makundi yote kupata elimu juu ya matumizi sahihi ya teknolojia kupata ujuzi stadi wa kidijitali ili kuchangamkia fursa zilizopo.

Ameyasema hayo katika kuanza kusheherekea Mwezi wa Wanawake dunia, Mbunge wa Viti Maalumu anayewakilisha Asasi za Kiraia(NGO's) Neema lugangila, jijini Dar es Salaam Machi Mosi, 2023, amesema kuwa wanawake wengi ni wajasiriamali na njia ya kupata masoko na wateja wengi na kupanua biashara ni kwa kupitia matumizi ya mitandao ya kijamii.

Akizungumzia Changamoto ambazo zinapelekea kufifisha jitihada za ushiriki wa wanawake mitandaoni ni pamoja na suala la ukatili wa kijinsia kwenye mitandao.

"Kwenye mitandao ya kijamii kunatabia ambayo imejengeka kwamba njia rahisi ya kunyamazisha, mkufifisha, kudogosha ajenda ya kiongozi mwanamke ni kwenda kwenye uzalilishaji wa kijinsia."

Akitolea mfano Mbunge Neema amesema... "Mimi naweka kitu kwenye mtandao mtandao wa kijamii ambao ninalenga ajenda fulani alafu anaibuka mtu au kundi kwasababu hawana hoja zenye mashiko au wanatafuta njia ya kudogosha kilichosemwa basi watahamisha ile hoja kutoka kwenye ajenda na kuingia kwenye ujinsia na pale ambapo wanawake wata tapopaza sauti basi watesema viongozi wanawake huwa hampendi kukosolewa, lazima mjifunze kukosolewa, na sisi tunachosema huko sio kukosoana huo ni udhalilishaji wa kijinsia, ni ukatili wa kijinsia kwenye mitandao."

Amesema kama mtu anashida na ajenda iliyopo au unamaoni tofauti na ajenda uliyosema ijadiliwe ajenda ikosolewe na ijadiliwe kwa hoja na kwa mkutadha wa ajenda ile lakini hoja huja isibadilike na kuanza kumjadili aliyeweka ajenda.

Akizungumzia mchakato wa sheria ya vyama vya siasa na mabadiliko ya sheria ya uchaguzi amesema kuwa sheria hizo lazima zifanyiwe marekebisho ili sheria hizo mbili zitambue ukatili wa kijinsia mtandaoni kama ni moja ya makosa mtandaoni ambayo yanaweza kupelekea zitambulike kama ukatili wa kijinsia mtandaoni ni makosa ambayo yanaweza kupelekea hata pale unapochaguliwa na chama chako uenguliwe.

"Kwasababu yapo makosa ambayo yanatambulika na sasa tunataka kosa la ukatili wa kijinsia kwenye mtandao nalo liwepo ili itakapotokea kama mtu anatabia ya kudhalilisha wanawake mtandaoni basi uenguliwe katika chama chake anachogombea." Amesema Mbunge Neema

Kwa Upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi, amesema katika mafunzo yanayoendeshwa katika mtandao huo amesema wamezindua mwezi wa Wanawake ikiwa mwaka kauli mbiu ya mwaka huu ni Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia

Amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga katika kumsaidia mwanamke katika nafasi ya mitandao ya kidijitali katika kuimarisha utendaji wa Uongozi kisiasa lakini pia katika upatikanaji wa fursa na kujipatia kipato wanawake wajasiriamali ili waweze kufaidi matunda ya ukuaji wa teknolojia nchini.

"Mwezi huu wa wanawake unaangazia nafasi ya Teknolojia katika Kuimarisha Wanawake na Uongozi na katika kuleta usawa wa kijinsia na katika kupunguza kero za kijinsia." Amesema

Amesema TGNP wanaendelea na matukio mbalimbali ya kuelekea kilele cha Siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika Machi 8, kila mwaka.

Amesema kuwa katika siku hiyo kutakuwa na kongamano ambalo litakuwa na majopo ambayo yatakuwa na mada mbalimbali ambazo zitatoa fursa katika ngazi ya kijamii na katika vituo ambavyo wanafanyanavyo kazi ikiwa ni pamoja na vituo vya Mafunzo na maarifa.

Amesema kuwa Wilaya zote nchini zitakuwa na maadhimisho ya siku ya wanawake katika maeneo yao pia watatumia mitandao ya kijamii na pia kutakuwa na sehemu salama kwaajili ya kuzungumza na wanawake waliobobea kwenye masuala ya tehama na Ubunifu.

Akizungumzia changamoto zinazowakuta watoto wakike katika Nafasi ya Teknolojia katika kuimarisha Wanawake na Uongozi, Mwanafunzi kutoka Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya na Naibu waziri wa Elimu na Taaluma, Davina Kaanani amesema kuwa amesema Wanawake wamekuwa wahanga wa mitandao ni mazingira hasa tamaa ya kupata kitu bila kujua madhara yake.

"Changamoto ni mwanamke akipost kitu cha kawaida anahofia kutokupata 'Likes nyingi na kupelekea 'kuposti' kitu ambacho kitapelekea kupata 'likes nyingi hasa za kudhalilisha utu wake." Amesema

Amesema kuwa mhemuko tamaa na vinapelekea kuwa wadada wengi kuwa wahanga sana katika ukuaji wa teknolojia.

Picha ya Pamoja.
Mbunge wa Viti Maalumu anayewakilisha Asasi za Kiraia(NGO's) Neema Lugangira, akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kuzungumza na wanajamii wa maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam Machi Mosi, 2023.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi akizungumza na waandishi wa habari Maci mosi katika kuanza kusheherekea mwezi wa wanawake.
Mwanafunzi kutoka Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya na Naibu waziri wa Elimu na Taaluma, Davina Kaanani akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Machi Mosi, 2023.
Mwanafunzi akiuliza swali.









Baadhi ya washiriki katika mafunzo ya uongozi na Teknolojia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad