HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 13, 2023

Maadhimisho Siku ya Wanawake Duniani, VETA Chang'ombe yatoa wito wa mafunzo

Mwanafunzi wa VETA Chang'ombe  Kozi ya Urembo Wastara Khamis akionesha umahiri wa kusuka kwa mwanafunzi mwenzake wakati maonesho  ya Bidhaa za Wanawake ikiwa Maadhimisho ya Siku Wanawake , Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Mwanafunzi wa Chuo cha VETA Chang'ombe wa Kozi ya  Elekroniki Evelyne Patrick akionesha ubunifu wa kifaa kinachoweza kufungwa katika Wodi za Hospitali kwa ajili ya kutoa ishara kwa Daktari kwenda kutoa huduma kwa mgonjwa wakati maonesho ya Bidhaa za Wanawake kwenye Siku ya Wanawake yaliyofanyika Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi wa VETA Chang'ombe  Kozi ya Maabara  Tamia Hussein  akionesha  dawa mbalimbali kuua wadudu walizotengeneza kwenye mafunzo katika chuo hicho   wakati maonesho  ya Bidhaa za Wanawake ikiwa Maadhimisho ya Siku Wanawake , Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Mtumishi wa Chuo cha VETA Chang'ombe Kozi Fupi Elizabeth Allen akizungumza na waandishi habari kuhusiana na Chuo hicho kinavyowaanda katika maafunzo ya Ufundi kwa makundi yote katika kwenda kwenye uzalishaji kwenye maonesho ya Bidhaa za Wanawake , Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya wanafunzi wa Chuo cha VETA Chang'ombe na Mtumishi wa Chuo hicho kwenye maonesho ya Bidhaa za Wanawake katika Maadhimisho  ya Siku Mwanamke Duniani , Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa Chuo cha VETA Chang'ombe wakiwa na bidhaa mbalimbali kwenye maonesho ya Bidhaa za Wanawake katika maadhimisho ya  Siku ya Mwanamke Duniani.

*Wataka wanawake wajikwamue kiuchumi kwa kufanya shughuli za kiuchumi kwa utaalamu ili kuongeza uzalishaji

Na Chalila Kibuda Michuzi Tv
CHUO cha VETA Dar es Salaam maarufu VETA Chang’ombe kupitia Maonesho ya Bidhaa za Viwanda vya Wanawake kimetoa wito kwa wanawake na wasichana kuchangamkia fursa za mafunzo ya ufundi stadi zinazopatikana chuoni ili waweze kujiajiri kwenye shughuli mbalimbali za ujasiriamali.

Wakizungumza katika maonesho hayo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani katika Viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho wamesema kuwa baada ya kufika chuoni na kuanza mafunzo wamepata mabadiliko kifikra ya kukamata fursa pale watapohitimu.

Mwanafunzi wa VETA Dar es Salaam kozi ya maabara Tamia Hussein amesema kuwa baada ya kusoma kozi hiyo ameona kuna fursa ya kutengeneza dawa za kuua wadudu chooni pamoja na utengenezaji wa sabuni mbalimbali ambapo mahitaji yake ni makubwa.

Tamia amewasihi wasichana ambao wako nyumbani pamoja na wanawake wajitokeze kwenda kusoma kutokana na ukweli kuwa kazi nyingi zinahitaji mtu kuwa na ujuzi ili kuajiriwa au kujiajiri.

Mwanafunzi wa Kozi ya Urembo Wastara Khamisi amesema kuwa shughuli za urembo zinaendelea kukua zaidi na wataalamu wake kuhitajika kwa wingi kwenye soko la ajira na kwamba mafunzo kwenye kozi hiyo yanamwongezea mtu uwezo na kufanya kazi hizo vizuri zaidi.

Amesema lengo lake atakapohitimu mafunzo yake ni kuanzisha saluni yake kutokana na mafunzo hayo na kutambua kila mtu ana urembo wake na sio kufanya kazi ya mazoea bila utaalam ambapo mwisho wa siku inakuwa kazi ya kubahatisha.

Mwanafunzi wa mwaka pili Fani ya Elektroniki Evelyne Patrick amesema katika mafunzo yao wamebuni kifaa kinachoweza kutoa taarifa kwa Daktari kwenye Wodi kuwa anahitajika kutokana na taa maalum.

Amesema kuwa ubunifu huo umebuniwa baada ya kuona changamoto inayowakabili wagonjwa pale wanapohitaji huduma ya daktari wodini.

Naye Mtumishi wa Chuo hicho Kitengo cha Kozi Fupi Elizabeth Allen amesema kuwa ushiriki wa chuo hicho kwenye maonesho hayo umelenga kuwashirikisha wanawake wajasiriamali juu ya fursa za mafunzo zinazopatikana Chuoni hapo zitakazoweza kuboresha zaidi shughuli zao na kuongeza uzalishaji na mapato.

Elizabeth amesema kuwa maadhimisho ya Siku ya Wanawake ni sehemu ya kutathimini vitu ambavyo mwanamke anafanya katika kujikomboa kiuchumi .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad