HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 10, 2023

Kenya Wavutiwa na DART Utoaji wa Huduma Usafirishaji wa Umma


Picha mbalimbali za Kaimu Meneja wa Mipango na Usafirishaji wa DART Mhandisi  Mohamed Kuganda akitoa maelezo kuhusiana na utoaji wa huduma za usafiri wakati Sekta ya Usafirishaji nchini Kenya ilipotembelea DART nchini Tanzania.

Kaimu Meneja wa Mipango na Usafirishaji wa DART Mhandisi Mohamed Kuganda akizungumza na Wadau wa Usafiri Nchini Kenya wakati walipotembelea Uwekezaji wa DART kwenye usafirishaji wa Umma jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Usanifu wa Usalama wa Barabara na Mazingira wa Kenya Mhandisi Ezekiel Wafula akizungumza namna walivyoona huduma ya usafirishaji wa Umma wakati walipotembelea DART jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Kaunti ya Mombasa Jeizan Faruk akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na usafirishaji wa Umma katika jijini Dar es Salaam wakati walipotembelea DART.


Picha ya pamoja ya  Wadau wa Usafiri kutoka nchini Kenya  wakiwa katika picha ya pamoja kwenye kituo cha Mabasi Yaendayo Haraka Ubungo Maji wakati walipotembelea DART jijini Dar es Salaam.

*Wasema Tanzania sehemu ya kujifunza kwa nchi za Afrika katika huduma za usafirishaji wa Umma

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
WAKALA wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) umesema kuwa mradi wa mabasi yaendayo haraka umekuwa kivutio baadhi ya nchi ya Afrika kuja kujifunza mradi wa usafirishaji wa Umma naamna unavyotoa huduma ya usafiri wa Umma huku wengine kutaka nchi zao kuwa na uwekezaji huo.

Hayo ameyasema Kaimu Meneja wa Mipango na Usafirishaji wa DART Mhandisi Mohamed Kuganda Niaba ya Mtendaji Mkuu wa wakati Wadau wa Usafiri kutoka Nchini Kenya walipotembelea Wakala hiyo kujionea huduma za usafiri wa Umma uendeshwa katika jijini la Dar es Salaam.

Mhandisi Kuganda amesema kuwa mradi wa mabasi yaendayo haraka kwa sasa ndio unakuwa na unatembelewa na mataifa mbalimbali namna wanavyoweza kutoa huduma ya usafiri unaofanya kuchochea uchumi wa nchi kutokana wananchi kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa urahisi kuliko kuwa na mabasi madogo madogo katikati ya Mji.

Amesema kuwa wakati wakitembelea mifumo DART wanapata picha kupitia mifumo mbalimbali ya uingizaji abiria ndani ya kituo pamoja na miundombinu.

Aidha amesema kuwa ziara ya Serikali ya Kenya katika Sekta ya Usafirishaji wameonesha nia ya kwenda kutekeleza nchini mwao katika kutoa huduma za usafiri wa Umma kwa wananchi.

Hata hivyo amesema kuwa licha ya kuwa kivutio wakala unaendelea kuboresha huduma za usafiri pamoja mifumo mbalimbali kutokana na teknolojia inabadilika kila siku.

"Mradi wa Mabasi umekuwa kivutio kazi yetu DART ni kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kwani hicho ndio kipaumbele chetu na tunasimama kwenye hicho kipaumbele hicho".amesema Kuganda

Mkurugenzi wa Usanifu wa Usalama wa Barabara na Mazingira Ezekiel Wafula amesema mfumo wa usafiri ni mzuri sana na kuonyesha picha kuwa hata Afrika vitu vipo vizuri.

Amesema kuwa nchi za Afrika zimekuwa zikijifunza kwa nchi zilizoendelea kwa sasa ni tofauti watu tunaweza kujifunza kwa nchi zetu ikiwemo Tanzania katika utoaji wa huduma za usafiri wa Umma.

Amesema kuwa DART imewapitisha kila hatua ya mradi wa miundombinu hivyo kazi yao ni kwenda kutengeneza mpango mkakati kuwa na mradi huo na kuongeza usafiri huo unapunguza hewa chafu inayosababishwa na mabasi mengi.

Katibu wa Kaunti ya Mombasa Jeizan Faruk amesema kuwa mradi huo Mombasa wakitekeleza watakuwa wamemaliza changamoto ya usafiri.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad