Na Mwandishi Wetu
KATIKA kuelekea
siku ya wanawake duniani mkoani Mbeya,Kampuni ya Oryx Gas kwa
kushirikiana na Mfuko wa Tulia leo wameandaa tamasha kubwa ambapo Oryx
Gas wameshindanisha vikundi 50 vya wanawake wanaojishughulisha na
biashara za vyakula kupika vyakula mbalimbali vya kiasili na washindi wa
kila kikundi wataondoka na zawadi ya majiko ya gesi na pesa jumla ya
shilingi milioni tano.
Hatua ya kuandaa mashindano hayo ya
vyakula kwa wanawake wanaojihusisha na biashara ya vyakula ni mojawapo
ya jitihada kampuni hiyo inafanya katika kuelimisha Watanzania kutumia
nishati safi ya kupikia kama mbadala wa kuni na mkaa.
Akizingumza
mkoani Mbeya kuelekea Siku ya Mwanamke Dunia ambapo wameamua kuandaa
mashindano hayo ya mapishi yaliyofanyika Machi 4,2023 , Meneja Masoko wa
Kampuni ya Oryx Peter Ndomba ameelezea kwamba kumekuwepo na madhara
makubwa ya kiafya,mazingira na kuichumi kutokana na jamii kutumia kuni
na mkaa katika kupikia.
Hivyo amesema moja ya jitihada
wanazofanya ni kuungana na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu
Hassan ni kuhakikisha watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ili
kuondokana na madhara na kuishi maisha bora.
"Tunaamini jitihada
ambazo tumekuwa tunazifanya pia ni katika kutekeleza nia ya Rais Samia
kuwa ifikapo mwaka 2030 angependa kuona zaidi ya asilimia 80 ya
Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia.Hivyo kwetu sisi tumeamua
kuyabeba maono ya Rais na Serikali yake Kwa vitendo.
"Kwani
tumekuwa tukitoa elimu kuhamasisha matumizi ya nishati ya gesi katika
kupikia na tumekuwa tukigawa bure mitungi na majiko ya gesi kwa wananchi
wa mikoa mbalimbali na leo tuko kwenye mashindano haya kwa lengo lile
la kuendelea kuhimiza matumizi ya nishati safi katika kupikia,"amesema
Ndomba.
Kuhusu ujumbe wao Kampuni hiyo kwa umma, Ndomba amesema
wanawaomba wananchi walinde sana afya kwa kuepuka matumizi ya nishati
chafu huku akifafanua katika kutoa hamasa mbalimbali wameanza kuona
mabadiliko hasa kwa yale maeneo yaliyoathilika na ukataji miti.
"Hivyo
basi tunazidi kuhamasisha wengi watumie gesi na ukweli ni kwamba Oryx
Gas tunajivunia sana kukubalika na pia kuaminika na jamii na hii
imetuwezesha kufikisha huduma sahihi ya gesi kila katika kila kijij cha
Tanzania Bara na Zanzibar."
No comments:
Post a Comment